mafanikio watu wasiofahamika wakijaribu kuteketeza kwa moto banda moja
la kuoneshea picha za video.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Costantine Massawe alisema tukio la
kwanza lililotokea majira ya saa 8 usiku katika Kanisa la Betham
lililoko eneo la Donge ambapo wahusika waliteketeza kwa moto jengo la
Kanisa dogo lililokuwa likitumika zamani na kisha kuingia ndani ya
Kanisa kubwa la sasa na kuviwasha kwa moto vitambaa vilivyokuwa
vimefunika madhabahu.
Massawe alisema:
Kanisa lililoteketezwa hapo lilikuwa la zamani ila sasa linatumiwa na
waumini wa Betham kwa ajili ya kufundisha watoto lakini ibada zote
zinafanywa kwenye jengo hilo jipya ambalo ndilo lililochomwa vitambaa
vilivyokuwa vimefunika madhabahu.
Aidha, alisema taarifa za kuchomwa Kanisa hilo zilitolewa na Sauli
Taminola mmoja wa waumini hao ambaye analala hapo Kanisani ambaye
anadai alishtuka kutoka usingizini mara baada ya kuona moto ukiwaka
madhabahuni ndani ya Kanisa.
Tukio jingine la usiku huo huo alisema liliripotiwa kuhusisha Kanisa
la Miracle Revival lililopo eneo la Makorora majira ya saa 9 za usiku
ambapo watu walidai walishituka usingizini na kuona moto ukiwaka
kwenye nguzo za Kanisa hilo ndipo wakapiga kelele za kuomba msaada.
Mchungaji ambae anaishi jirani na kanisa alisema aliona watu wakiwasha
moto magurudumu (matairi) ya baiskeli na kuyafunga kweney boriti za
kanisa ili ziweze kuungua moto lakini baada ya kuwakurupusha jaribio
hilo lilishindwa kwakuwa moto ulidhibitiwa na watu pasipo kuleta
madhara makubwa
alisema Kamanda Massawe.
Akizungumzia klabu ya pombe za kienyeji iliyoteketea usiku huo alisema
tukio hilo lilitokea katika eneo la Kwanjeka kwenye baa inayofahamika
kama 'Bongola' na kudai kwamba chanzo ni shoti ya umeme.
Kamanda Massawe alisema tukio la nne limehusisha banda moja la
kuoneshea mikada ya picha za video huko huko Kwanjeka ambalo nalo
lilikaka kuteketezwa kwa moto na watu wasiojulikana lakini jaribio lao
halikufanikiwa.
---
Taarifa via Lukwangule Ent. blog
Source: http://www.wavuti.com/4/post/2013/05/tanga-makanisa-mawili-yachomwa-moto.html#ixzz2TjbmEoC6
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments