[wanabidii] ya kibanda YANAKERA kiukweli

Thursday, April 18, 2013
poleni sana wanahabari wenzangu kwa magumu mnayoyapitia.

haihitaji kwenda shule kujua habari ya kuwa makontena ya siraha yanaingizwa hapa kwetu ukerewe katika chuo cha ugaidi kuwa si ya kweli... habari ile ilizua hofu kubwa sana na masikitiko kwa jamii ya hapa kwetu UKEREWE... kwa kweli wahariri wa MTANZANIA mnatakiwa kujitahmini maana lengo la kupashana habari sio kuzua hofu wala migongano ndani ya jamii.

siku moja baada ya ile habari kutoka nilikaa katika kijiwe cha wazee wanapokutana kila jioni kunywa kahawa mzee mmoja alisema magazeti ni wapuuzi kontena haliwezi kuingia UKEREWE zaidi ya saa moja usiku, akimaanisha usafiri wa kuingia na kutoka  ukerewe hauwezi kufanyika labda serikali ndio iingize, tuna meli zinazotoka mwanza mbili na kurudi na zinafanya kazi mchana tu, kivuko cha kisolya mwisho saa kumi na mbili jioni, hakuna uwanja wa ndege huku.... hizi fact za mtu amabaye hajasomea taaluma yoyote chini ya jua.

habari kama hizo bila kutumiwa na baadhi ya watu wenye kutumia fedha  zao chafu mwandishi na muhariri timamu anayejua kazi yake hawezi kuiweka hewani,

sasa pengine watu kama akina KIBANDA wanakumbwa na majanga kama hayo kwa ujinga wa baadha ya waandishi wanaoaandika uzushi kwa kutumia cheo cha na MWANDISHI WETU matokeo yake wasioweza kujisumbua kwenda mahakamani wanamtafuta anayejulikana katika chombo husika... mfano wanaojulikana hapo new habari ni kibanda na barere wengine hawajulikani kabisa ukiondo Bashe labda.

.
GAZETI lingine kirahisi rahisi tu likaandika KIBANDA ameponzwa na mambo matatu (UNYAKYUSA WAKE, UKRISTO WAKE na nyingine siikumbuki) kwa kuwa mtu hajui madhara ya chuki me ni muhanga wa hayo yote matatu aliyoyataja mwandishi huyo..... roho ilikuja kutulia baadha ya saa kama sita hivi nilipokumbuka taaluma ya habari ilinifunda kitu gani nikiwa nasomea taaluma hiyo, nikajua aliyeandika na aliyeruhusu taarifa ile ikae front page ni MAJUHA wa taaluma na wamevamia fani hiyo,,,,, lkn leo tena naona wale wale aisee inakatisha tamaa tuombee tuendelee kuwa na serikali hii iliyolala lakn akija kichaa na anayejua maadili ya taaluma hiyo tutafungiwa na kufikishwa mahakamani kila kukicha.

   poleni waandishi, sasa geukieni ukweli nao utawaweka huru kwelikweli

Share this :

Related Posts

0 Comments