[wanabidii] Taifa limepoteza Uhuru

Friday, March 22, 2013
Taifa lipo njia panda likiweweseka,na hatari kuu za maangamizi.Nchi
imekosa dira na mwelekeo wa maendeleo,uchumi wan chi
umelala.Tunaimbishwa wimbo wa ujamaa huku tukichezeshwa ngoma ya
Ubebari.Taifa linakabiliwa na umomonyokaji mkubwa wa maadili na
utamaduni,nchi inabugia makapi na sumu ya kila aina kwa maangamizi
yake yenyewe.Taifa bila utamaduni na maadili yake ni sawa na mti bila
mizizi.Heshima ya mtanzania ndani nan je ya nchi imetoweka,udini
umeshika kasi,na hata kutishia kuigawa nchi katika vipande vipande
Watanzania tumepokwa haki na uhuru wetu wa kitaifa,kwa maana ya
kujitawala na hatma yetu bila kuingiliwa na watu wasio
wazalendo,tumepoteza uhuru dhidi ya magonjwa,uhuru dhidi ya njaa,uhuru
wa kiuchumi.Kupotea kwa uhuru huu ni matokeo ya uchumi na rasilimali
za nchi kumilikiwa na kikundi cha watu wachache,huku serikali dhaifu
ikisalimu amri kwa genge hili la wahujumu wachache.
Watanzania wamepoteza uhuru binafsi,haki ya kuishi maisha ya
heshima,haki ya kupata habari,usawa kwa wote.Eee Mtanzania amka kuwa
sehemu ya mabaliko utakayo……………………
"Kuna nyakati unaweza kuchoka kupinga dhulma na uonevu katika
jamii,lakini kamwe isitokee nyakati ukaacha kupinga dhulma na uonevu
katika jamii"
--
Ephata Nanyaro
P.o.box 15359
Arusha
+255 754 834152
Skype.nanyaro.ephata

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments