[wanabidii] Neno Fupi La Usiku Huu; Mchoyo Akizidisha Uchoyo Mwisho Hulala Na Njaa!

Friday, March 08, 2013


Ndugu zangu,
Uchoyo ni hulka ya mtu. Uchoyo si jambo jema. Na mchoyo akizidisha uchoyo wake mwisho hata yeye mwenyewe hulala na njaa.

Maana,itatolea nyumbani kwake atafika mgeni aliyeshiba. Mchoyo ataona tabu kupika chakula na mgeni naye ale. Anaweza kuhangaika na vikombe vya chai akisubiri mgeni wake aondoke.

Usiku mwingi utaingia, mgeni ataomba alale kwa mwenyeji wake. Mchoyo ataona aibu kumnyima hifadhi mgeni wake.

Lakini, kwa vile ana hulka ya uchoyo, na anaona tabu kupika chakula na mgeni wake naye ale, basi, mchoyo naye anaweza kulalia kikombe cha chai huku mgeni wake akiwa amelala na shibe!

Ni Neno La Usiku Huu. ( Pichani ni chai yangu ya usiku huu, HAIHUSIANI na Neno hili!)
Maggid,
Msamvu.
http://mjengwablog.co.tz

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments