[wanabidii] MGOGORO BAINA YA AIRTEL NA WAFANYAKAZI WA IDARA YA HUDUMA KWA WATEJA

Saturday, March 23, 2013
MAELEZO YA MGOGORO BAINA YA WAFANYAKAZI WALIOACHISHWA KAZI NA MWAJIRI
(AIRTEL)
IDARA YA HUDUMA KWA WATEJA

Historia,
Wafanyakazi wanaohusika na mgogoro huu idadi yao ni 179, ambao
waliajiriwa kwa vipindi tofauti kuanzia mwaka 2001 mpaka 2011.
Wafanyakazi hawa waliajiriwa na kampuni ya Celtel, wengine Zain na
wengine Airtel kwa masharti ya kudumu.

Celtel ilipoiuzia Zain kampuni, na Zain ilipoiuzia Airtel pia,
wafanyakazi hawa walichukuliwa bila kubadilishiwa chochote, wala
kusaini mkataba wowote wa ziada kwani masharti yaliendelea vile vile.

Mnamo tarehe 31 Machi 2011 Airtel iliwaachisha kazi wafanyakazi hawa
179, na kuwapeleka SPANCO RAPS, ambayo ni outsourced company inayotoa
huduma ya Customer Service kwa Airtel, katika mkataba wa makubaliano
baina ya Airtel na waajiriwa, ilikubalika kwamba mfanyakazi atabaki na
haki zake zote, na iwapo kutakuwa na kutoridhika katika utekelezaji wa
mkataba, mwajiriwa atakuwa HURU kurudi kampuni yake (Airtel) muda
wowote (mkataba huo umeambatanishwa).

Chanzo cha mgogoro

Mgogoro wa sasa ulianza baada ya wafanyakazi kukaa na mwajiri wa sasa
(Spanco) kuuliza haki za malipo ya kuachishwa kazi Airtel, baada ya
Spanco kuwakana wenzao walioachishwa kazi kwamba hawana haki ya kudai
fidia ya kuachishwa kazi kwa kuwa walikuwa wameajiriwa tarehe 1 April
2011, haki za nyuma zote hawazitambui wakamdai mwajiri wa zamani
(Airtel) katika migogoro wa kazi No CMA/DSM/KIN/800/11 na mwengine
CMA/DSM/KIN/737/11/788 . hatua hii ilileta hofu kwa wafanyakazi. Pia
kuna wafanyakazi walifukuzwa lakini hawakufungua migogoro ya kazi.

Kutokana na hali hiyo, wafanyakazi waliamua kuuliza kwa mwajiri wa
sasa kuhusiana na hilo, ambaye alikana kwamba hawezi kutoa haki hiyo
isipokuwa kuanzia 1 April 2011. Hivyo haki zote za nyuma zilifutwa kwa
mujibu wa mwajiri wa sasa. Hata hivyo wafanyakazi waliamua kwenda kwa
mwajiri wa zamani (Airtel) kuhusu hiyo haki, bahati mbaya hakuonesha
kujali. Email ya mwanzo haikujibiwa, mpaka ilipotumwa tena ndipo
ikajibiwa, hata hivyo mwajiri hakuonesha kujali madai ya wafanyakazi.
Kuona wanadharaulika, wafanyakazi waliamua kuandika barua tarehe…….
kwa mwajiri kukumbushia madai yao, naye alijibu tarehe…… . Wafanyakazi
hawakuridhika, hivyo kwa nia njema wakaomba mkukato na mwajiri wa
zamani ambapo tarehe ….. walikwenda wawakilishi wa wafanyakazi mpaka
makao makuu ya Airtel kwa majadiliano. Makubaliano hayo yaliyofikiwa
siku hiyo ni kwamba mwajiri atoe Certificate of Service, hata hivyo
mwajiri alikataa kulipa Severance entitlement.

Baada ya kuona hatua ya majadiliano haina mafanikio, wafanyakazi
waliamua kufungua mgogoro namba CMA/DSM/KIN/R.61/13 hatua ya
Mediation, ambao ulisikilizwa kwa mara ya kwanza tarehe 4 Machi 2013.
Mbele ya Mediator, mwajiri alikiri kudaiwa hela hiyo, akaahidi kwamba
kwa kuwa wafanyakazi ni wengi, anaomba muda akapige mahesabu na tarehe
20 Machi aweze kutoa msimamo. Pande zote zilikubaliana. Ilipofika
tarehe 20 Machi mbele ya Mediator, mwajiri alipotakiwa atoe msimamo,
kwa mshangao wa wafanyakazi na mediator, alikana ahadi yake ya tarehe
4 Machi, akidai kwamba hawezi kuwalipa wafanyakazi haki ya kuachishwa
kazi kwa kuwa amehamishia kwa mwajiri wa sasa. Hata hivyo katika
maongezi ilionekana hakuna maelezo yanayothibitisha haki hiyo kwenda
kwa mwajiri wa sasa.

Baada ya uamuzi huo, ilionekana kwamba hakuna njia nyingine zaidi ya
kurudi katika mkataba, na kipengele cha 3 cha makubaliano ya mwajiri
na mwajiriwa kinatoa uhuru kwa mwajiriwa kurudi katika ajira yake
iwapo hataridhika na hali ya utekelezaje wa mikataba. (Mkataba huo
umeambatanishwa). Hata hivyo kwa kuwa vyombo vya habari ni muhimu
kutoa taarifa kwa umma, wafanyakazi wameona ni muda mwafaka
ikizingatiwa kuwa Airtel hawaoneshi dhamira njema kutekeleza
makubaliano ya mkataba, hivyo tarehe 27 Machi wafanyakazi wamedhamiria
kurudi iwapo katika kesi yao Airtel hatoridhia kulipa.

Angalizo – Wafanyakazi wamefikia uamuzi huu kwa kuwa mwisho wa mkataba
wa maridhiano ni tarehe 31 Machi 2013 miaka miwili tangu tarehe 1
April 2011, hivyo iwapo watachelewa watapoteza haki yao.

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments