[wanabidii] Kagasheki Jr Amerudisha kadi ya CCM na kuhamia CHADEMA

Friday, March 01, 2013
Kutokana na juhudi za Kamanda Mawazo Alphonce alieko Mkoani Kagera kwa ajili ya M4C,
jana jioni familia ya Kagasheki imehamia Chadema. Mdogo wa Waziri Hamis Kagasheki anaeitwa Mbubarak Kagasheki pamoja na nduguye mwengine walimkabidhi kadi zao za CCM kamanda Mawazokwenye uwanja wa Rwamishenyi. 
Hotuba ya Mawazo iliwafanya watu kutokwa na machozi ya uchungu dhidi ya mfumo uliopo.
Diwani wa moja ya kata za mjini Bukoba alilia hadharani na kusema mara ya mwisho alilia machozi baada ya kusikia hotuba ya Mtikila.
Kada mwingine toka CUF anaejulikana kama Zainabu nae alirudisha kadi yake. Mpaka saa moja kasoro watu waligoma kuondoka uwanjani. 
Wananchi walimchangia Kamanda Mawazo takribani sh. 200,000.
Leo hii, Mawazo na timu yake (Husna na Hamis) wanahamishia ziara Karagwe kwa ziara ya siku 5.   
 
Fred 
MATURITY does not come with age, it begins with acceptance of Responsibility
Change is Essence to maturation 

Share this :

Related Posts

0 Comments