[wanabidii] Bodaboda wanapovunja sheria mbele ya Trafic

Tuesday, March 19, 2013
Kuna jambo huwa linanitatiza sana. Unakuta Trafic anaongoza magari  kwenye mataa
na mbele ya magari zipo pikipiki kibao ambazo zinachomoka moja baada ya nyingine mbele yake tena upande tofauti na ule anaoruhusu magari kupita wala hao Trafic hawastuki wala kuzuia wala kukemea naona wameshafanya mazoea. Je inamaana hao bodaboda hawatakiwi kufuata sheria za barabarani? na hao Matrafic watuambiie kwanini hawawachukulii hatua hao madereva wa pikipiki? au mpaka litokee janga kama la jana ndio Wakuu wa polisi wanasema hiyo ni changamoto. Please chukueni hatua mzaha mzaha hutumbua usaha.

Share this :

Related Posts

0 Comments