[wanabidii] UNYANYASAJI WA JINSIA KIGOMA

Monday, February 18, 2013
Si rahisi kuamini katika karne hii ya 21 kuna unyanyasaji wa kijinsia tena katika wizara nyeti ya selkari . Sikuamini kuwa viongozi wa asikari pollisi wanawapanga akina mama wanaonyonyesha katika marindo ya usiku au doria za usiku kwa kuwaambia kuwa hata wao wanapata mshahara.

Ndugu zangu nalaani kitendo hicho nanyi wana jamii niungeni mkono. Akina mama ndio mama zetu, hivi kweli hao watoto wadogo wanaonyonya tunawatendea haki kwa kuwalaza mbali na mama zao? Tunajisikia sawa tukilala ndani ya nyummba zetu huku watoto wanalia kwa kuwakosa mama zao?

Hivi kweli kamanda wa Polisi kigoma huwezi waonea huruma hao akina mama wanyonyeshao? Fikiria angekuwa ni mkeo au dada yako ananyanyaswa hivo.

Chonde chonde bwana RPC Kigoma tatua hilo tatizo, hata kama ulifanya kwa nia njema basi fikiria kwa undani ubadiri msimamo.

Ahsante

Share this :

Related Posts

0 Comments