[wanabidii] TAMKO LA TGNP KUPINGA KUZUIWA MATANGAZO YA LIVE BUNGENI NA KUFUTWA KWA POAC

Wednesday, February 20, 2013
*TAMKO KWA VYOMBO VYA HABARI*

*KUSUDIO LA KUZUIWA KWA MATANGAZO YA MOJA KWA MOJA KUTOKA BUNGENI –
DODOMA
NA KUFUTWA KWA KAMATI YA HESABU ZA MASHIRIKA YA UMMA (POAC)*

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) ni shirika linalotetea na kupigania
haki
na usawa wa Kijinsia, ukombozi wa wanawake kimapinduzi, haki za
Binadamu.
Tumepokea kwa masikitiko taarifa za ofisi ya Bunge la Jamhuri ya
Muungano
wa Tanzania kuwa ina utaratibu wa kuzuia matangazo ya moja kwa moja
kutoka
Bungeni (LIVE) wakati vikao vya Bunge vinapoendelea, na baadaye
vitarushwa
baada ya kuhaririwa na kufutwa kwa kamati ya Bunge ya Hesabu za
Mashirika
ya Umma (POAC).

Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashillilah amesema kuwa vikao vya Bunge
havitarushwa moja kwa moja na runinga. Sisi TGNP tunasema kuwa
Wananchi
wana haki ya kufuatilia mijadala inayowahusu, ikiwemo Vikao vya
bajeti,
miswada ya sheria na hoja mbalimbali za wananchi yakiwepo maswali ya
wabunge kwa serikali juu ya kero na mahitaji ya wananchi.

Serikali ya Tanzania imeridhia Tamko la Haki za Binadamu, Desemba 10,
1948
ambapo Kifungu cha 19 cha tamko hili (Article 19), kinatoa uhuru wa
mtu
kutoa na kupokea mawazo bila kujali mipaka ya nchi na haki hii ya
kutoa
mawazo haipaswi kuingiliwa. Kwa kitendo hiki serikali inavunja tamko
hili.

TGNP tumestushwa sana na Kitendo cha Spika wa Bunge, kuifuta Kamati
ya
POAC, ambayo imekuwa na ufanisi mkubwa katika kudhibiti mianya ya
ufisadi
katika sekta ya umma.

Tunalaani kitendo cha kuifuta Kamati hii na sisi kama wanajamii
tutaendelea
kudai ulinzi wa rasilimali za Taifa hili na Bunge linapaswa
kutuwakilisha ipasavyo katika kudai uwajibikaji wa watendaji wa
serikali.

Kwa hiyo Kamati ya POAC ni muhimu na irudishwe. Tanzania ina jumla ya
Mashirika ya Umma 258 yenye dhamani ya sh. Trilioni 10.2, tunahitaji
kamati
ya Bunge makini ya kunusuru rasilimali hizi, la sivyo kwa vyovyote
vile
Taifa linarudi miaka ya kabla ya 2008, ambapo wizi wa EPA, MEREMETA,
RICHMOND na ubinafsishaji holela wa mashirika ya umma ulifanyika.

Kutokana na kusudio hili la Ofisi ya Bunge, sisi wanaharakati wa
Mtandao wa
Jinsia Tanzania (TGNP), tunatamka kuwa:

v Vikao vya Bunge viendelee kurushwa kama kawaida na wananchi
wafuatilie
kama ilivyokuwa hapo nyuma.

v Ofisi ya Bunge (kiti cha Spika) wakiheshimu sheria, kanuni za
kudumu za
Bunge na haki ya wananchi ya kupata habari iliyoainishwa kwenye tamko
la
Haki za Binadamu Kifungu cha 19.

v Ofisi ya Bunge kutoingilia mijadala ya wabunge na serikali hasa
wabunge
wanapodai uwajibikaji wa serikali kwa wananchi wake, ikiwa ni pamoja
na wajibu
wa serikali kutoa huduma za msingi za kijamii kwa wananchi kama maji,
elimu, afya, miundombinu nk.

v Tunamtaka Spika wa Bunge kufanya maamuzi kwa kuzingatia maslahi ya
nchi
na historia ya uwajibikaji katika nchi.

v Waandishi wa habari waendelee kuwapiga picha wabunge wanaolala
usingizi
Bungeni ili wananchi waone aina ya viongozi wanaowapeleka Bungeni na
kutokuwachagua tena kipindi kijacho.

v Kuzuia matangazo ya TV ni kukaribisha ufisadi, kuongeza utoro
Bungeni na
maovu mengine kufanyika kwa usiri kinyume na matakwa ya wananchi
waliowatuma
wabunge.

v Tunamtaka Spika wa Bunge kuirudisha mara moja Kamati ya POAC kabla
ya
Mkutano wa 11 wa Mwezi April 2013.

Ofisi ya Bunge na Spika lazima zielewe kwamba Mamlaka yapo kwa
wananchi na
wao ni wasimamizi tu wa vikao vya Baraza la wananchi liitwalo Bunge.
Wananchi
ndio wenye mamlaka ya mwisho!

Imetolewa na:
* *
* *
*Lilian Liundi*
*Kaimu Mkurugenzi Mtendaji TGNP*

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments