Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi itafanya Mkutano
wake wa kawaida kuanzia tarehe 10-11 /02/2013. Kikao hicho kitaongozwa
na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.
Wajumbe wa NEC wanatarajiwa kufika Mjini Dodoma leo tarehe 9/02/2013,
kwa ajili ya kikao hicho.
Pamoja na mambo mengine kikao hichi kitatanguliwa na Semina ya siku
mbili kwa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa.
Lengo la Semina hii ni kuwaongezea Wajumbe uelewa kuhusu masuala ya
Chama Cha Mapinduzi na Serikali yake hasa ikizingatiwa kwamba wengi wa
Wajumbe ni wapya kufuatia Uchaguzi Mkuu wa CCM wa mwaka 2012.
Mada zitakazowasilishwa kwenye Semina ni pamoja na;
1. Nafasi na Wajibu wa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa
2. Umuhimu wa Maadili kwa Viongozi na Watendaji wa Chama Cha
Mapinduzi.
3. Mikakati ya kutekeleza maazimio ya Mkutano Mkuu wa Taifa wa nane wa
CCM.
4. Mkakati wa kukuza ajira nchini.
Semina hii itafuatiwa na Mkutano rasmi wa Halmashauri Kuu ya Taifa
ambao pamoja na mambo mengine utafanya Uchaguzi wa Wajumbe wa Kamati
Kuu ya Chama Cha Mapinduzi.
Imetolewa:
Nape Moses Nnauye
KATIBU WA NEC – ITIKADI NA UENEZI
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments