[wanabidii] NUNUA KIWANJA KIDOGO CHENYE RUTUBA KULIKO KIKUBWA KISICHO NA RUTUBA

Wednesday, February 20, 2013
SERIKALI NUNUA KIWANJA KIDOGO CHENYE RUTUBA KULIKO KIKUBWA KISICHO NA
RUTUBA KWANI GHARAMA HUTOIWEZA.

Mjomba nami leo wacha nimwage cheche zangu kwa hili serikali imekosea
ila siilaumu ijipange upya tuu ndo kuangalia "nini chanzo".

Ninasikitika sana lakini kwa sababu haina jinsi inabidi nikubali tuu
na kisha nicheke japo kidogo. Kwa nini hawa wahusika hawawajibishwi,
hadi inafikia tunafika kiwango hiki. Takwimu hadi leo sijaziamini ila
inabidi nikubali tuu kuwa katika kila wanafunzi 100 basi sitini ni
maziro. Ikimaanisha katika kila wanafunzi mia waliofanya mtiani wa
kidato cha nne, sitini kati yao hawakuwa na uwezo wa kufanya mtihani
huo. Tulikuwa tukisikia kuwa shule za kusini zinafeli au shule za
serikali zinafeli haya yote yamekuwa ni tabia sasa na hakuna
ufuatiliaji wowote ule. Sasa ugonjwa ushaambukiza na kwingine hivyo
dawa sijui itakuwaje maana chanjo hamukutoa kwa waathirika wa miaka
iliyopita.

Serikali inapanga 20% ya bajeti au mijihela kwa ajili ya masuala ya
kielimu ila wanafunzi wanapata "mabuyu" au wanataga. Inasikitisha ila
inafurahisha kwa upande mwingine kwamba serikali badala ya kuangalia
"Quality" yenyewe inaangalia "Quantity" nikimaanisha badala ya
kuangalia viwango au elimu bora wao wanaangalia idadi. Hii ni sawa na
kununua eneo kubwa unaloambiwa halifai kwa kilimo na kuliacha eneo
dogo lenye kina aina ya mahitaji kwa ajili ya matokeo mazuri au kilimo
bora.

Ifikie wakati sasa walimu wanapotoa hoja zao wasikilizwe. Haiwezekani
kuwa mwalimu analalamika na maisha pia yanamkandamiza, mwenye nyumba
anataka kodi, watoto walipiwe ada, bado hajaumwa nk. Kisha anapoteza
muda wake ili aweze kuongea na wewe kisha unayachukulia malalamiko
yakekirahisi rahisi tuu na kuyatia kapuni. Maswali yao hayajibiwi,
matakwa yao hayatekelezwi unategemea nini hapo.

Hebu tuchukue mfano mdogo kuwa mimi nimesoma Dar tangu elimu ya msingi
hadi namaliza chuo na degree yangu ya ualimu. Nimepigika sana, sina
historia ya kuishi nje ya Dar kisha wewe unanipangia kazi Rufiji,
Musoma au mikoa mingine ambayo ukitaka mahitaji muhimu basi upoteze
siku nzima kuyafuata, kisha unaniacha nijitegemee mwenyewe hapo
nitaishi vipi na nikikuambia kuna masuala tuongee husikilizi.
Kifuatacho ni kuhamia shule ya private kwa kurudi Dar au kutafuta
biashara nifanye kuliko kwenda shule wakati hainisaidii kimaisha. Si
kwa wote ila kwa wengi mtu ataangalia maisha yake kwanza haiwezekani
yeye aumie kisha awanufaishe wengine hiyo imani tulishaiacha zamani na
si utamaduni wetu tena.

Inasikitisha kuwa wanafunzi waliofikia kiwango cha kuingia kidato cha
Tano ni asilimia sita "6%" au wanafunzi 23,520 na wanafunzi 344230
hawana kiwango. Bora serikali itoe tena matokeo ili "wayastandardize"
au wayasanifishe walau B iwe A, C iwe B na kadhalika lakini kwa hili
sijui wapi tunaenda. Inaniuma sana nikifikiria hasa kuwa kuna kundi
kubwa sana ambalo halina tena muelekeo wowote hususani wenzangu na
mimi wasio na uwezo wa kifedha wa kurudia mitihani au kwenda private
schools.

Kwa form four wapya muda munao na jitahidini kujipanga kaka yenu hapa
Ally Malaptop nawatakia maandalizi mema muda bado munao.

Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2LU9gqeei

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments