Ndugu zangu ,
Ni miaka 3 sasa toka mwaka 2010 tulipotoka kwenye uchaguzi mkuu Nchini ambapo chadema ilipata wabunge wengi zaidi kulinganisha na vyama vingine vya upinzani nchini haswa upande wa Tanzania bara .
Katika miaka hii hatujasikia wala kuona uongozi wa CHADEMA ukiongelea suala la kuachiana uongozi zaidi ya wale wenye nia ya kugombea nafasi Fulani ndani ya chama hicho wakishambuliwa au kuonekana mamluki , wengine kufukuzwa chama na hata wengine kutishiwa kufukuzwa .
Wakati CHADEMA kukiwa hivyo ndani ya CCM kumefanyika mabadiliko kadhaa kuanzia NEC ,UWT ,UVCCM , Viongozi wa Wilaya na Mikoa wengine tumeona wakiondolewa kwenye nafasi wengine wakiondoka wenyewe .
Kuhusu kuutaka urais tumesikia baadhi ya majina yakitajwa toka CCM lakini hatujawahi kusikia baadhi ya wanachama wa CCM wakitukana wenzao wenye nia ya kugombea urais kupitia chama hicho mara kadhaa tumeona wakishindana kwa hoja .
Ni wakati sasa kwa CHADEMA kama chama kukuu cha upinzani kuanza harakati za kuwaachia uongozi wanachama wengine wa chama hicho wenye uwezo zaidi na mikakati endelevu kuelekea mwaka 2015 na hilo lianze sasa hivi sio kwa kufukuzana .
www.wejobs.blogspot.com Jobs in Africa
www.jobsunited.blogspot.com International Job Opportunities
-- Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments