[wanabidii] KATIBU WA TFF AWA KITUKO

Monday, February 18, 2013
Jana usiku TBC ilirusha mahojiano kati ya Katibu wa TFF (ANYITILE),
Michael Wambura na wadau wa soka
hapa Tanzania. Michael Wambura alieleza namna viongozi hao wa TFF
walivyobadili Katiba ili ikidhi matakwa binafsi kinyume na katiba ya
TFF kwa kurejea vifungu vya katiba ya TFF.

Kinyume na wambura, katibu huyo alibaki kueleza blablaa tu bila hata
kuwaambia watazamaji na washiriki ni vifungu gani
walitumia kubadili katiba na hatimaye kuwaengua baadhi ya wagombea.
Kituko kilikuwa pale katibu huyo alipoulizwa maswali
na washiriki pamoja na wasikilizaji ni kwa nini baadhi ya wagombea
walionekana wanafaa kipindi kilichopita na sasa inaonekana hawafai.

Muda wote alikuwa akitokwa na maneno mithili ya mtu mwenye ugonjwa wa
akili akijibu chochote bila kujali swali aliloulizwa akimshambulia
Wambura. Binafsi nilimuona yeye na boss wake Tenga aliyekuwa
ametangulia kuongea na vyombo vya habari siku moja kabla kama hawana
sababu yoyote ya msingi ya kuwaengua wagombea isipokuwa ni
uchakachuaji tu. Nina wasiwasi mahesabu yao ya fedha humo ofisini
hayajakaa vizuri, ni vyema kabla ya kukabidhi ofisi kwa viongozi
watakaochaguliwa ifanyike special audit kubaini chanzo cha woga
walionao kwa baadhi ya wagombea. Kama kungelikuwepo na sababu za
msingi asingekosa majibu yanayoeleweka. Kwa mtindo huu soka la bongo
halitafika popote

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments