[wanabidii] MASWALI YALIYOACHWA NA WAANDISHI KWA JULIANA SHONZA

Wednesday, January 16, 2013

Juliana Shonza ameshauriwa vizuri sana na Uwezo wa washauri wake umejulikana wakae washauriane kujibu haya.

1.      Kama anajua kuwa yeye ni Makamu Mwenyekiti wa Bavicha, kwanini asiende ofisini kufanya kazi, badala yake anahangaika kuwaita waandishi kuwaarifu kuwa yeye ataenda Mahakamani. Anashtaki nini wakati anasema hajafukuzwa?. Makamu Mwenyekiti haiti vikao hotelini, kwanini hakuita kikao Makao Makuu ya Chama wakati anajua hajafukuzwa?

 

2.      Analalamika hana barua ya kufukuzwa, wakati humu kwenye JF yeye na wapenzi wake ndo wameileta hapa hii aliyoleta hapa ameipata wapi? Amejiandikia?.

 

 

3.      Anatumia hoja ya mshahara wa Dr. Slaa, hiyo mbona ilitumika wakati wa kampeni CCM ndo walikuwa wanalalamika, yeye alishiriki uchaguzi au hakushiriki? Alijua ajenda za CCM? Hii ajenda ya CCM kuhusu mshahara wa Slaa anaileta kwa akili yake au kwa kutumwa?

 

4.      Vijana waliomchagua ndio waliomfukuza, anajisifu vijana wepi wengine? Aliwadharau akiwa Morogoro akatoka katika kikao chao, kamati ikaundwa afike kuhojiwa akatoa matusi, akasaidiwa na Mchange kujibu barua kwa kamati ambapo angefika kujieleza.

 

 

5.      Mbona hasemi kuhusu meseji na kijana wa CHASO ambaye amekuwa akichukua hela kwa shibuda halafu akaenda kumhonga ili atoea tamko kuchafua viongozi wa Chama.

 

6.      Hata kama Baraza la vijana halikutendeka haki, je amekorofishana na uongozi wa juu wa Chama tangu lini, mbona ni mahali ambapo kama hatumiki na CCM ndo angekata rufaa akajieleze? Lakini ameanza kuwashambulia?

 

 

7.      Je Hoja ya kufukuzwa uanachama wa Bavicha ilianza na "upuuzi" anaousema kuhusu Mbowe na Dr. Slaa au zilianza na kashfa zake na mdhamini wake Shibuda? Kwanini hoja ya Dr. Slaa na Mbowe zije wakati ameshafukuzwa?

 

8.      Kama alikuwa na Madai mazito hivi kwanini hakuyasema kwenye Chama, au kamati iliyoundwa ili aone kama angepuuzwa ndo aje kwa waandishi, kuwajulisha watanzania?

9.      Anasema kuwa Heche hakuwa na sifa ila alibebwa, je kama Heche alibebwa alikubali vipi Shonza kuwa Makamu kwa Mwenyekiti asiye na sifa? Na kwanini amefanya kazi naye kwa muda wote bila kutoa malalamiko, hadi Heche alipokataa kukubali JK kuwa Meneja wa Kampeni kwa Mgombea wa CHADEMA mwaka 2015, na pia Mgombea huyo kutangaza nia kwenye mkutano wa CCM?

 

10.   Katika tuhuma zote, angesema yeye alikuwa analipwa kiasi gani kama Heche alipendelewa, Lakini hao wenyeviti wa mikoa anaodai hawalipwi hawalalamiki na ndio wamemfukuza yeye anayejidai analalamika kwa niaba yao, je wao hawataki pesa?

 

 

11.  Kuita kamati tendaji ya Bavicha kuwa ni kikundi cha "kihuni" na wewe bado unasema ni Makamu mwenyekiti, je yupo tayari kukiri kuwa yeye ni kiongozi wa kikundi cha kihuni? Kwanini amekuwa akiongoza kikundi cha kihuni?

 

12.  Anajidai, anaijua katiba, kwanini alipoitwa kwenye kamati alisema anataka aandikiwe barua kuombwa na Dr. Slaa ili akahojiwe na kamati. Hiyo barua ilihusu nini?. Lakini pia kuzungumzia uhai wa Wanachama, Mwampamba, Mchange, yeye anasema hajafukuzwa, je alijuaje kuwa Mwampamba na Mchange wamefukuzwa? Kwa barua ipi? Na je utaratibu wa unachama katika Chadema unatokana na matangazo ya viongozi na vikao na waandishi wa habari?

 

13.  Shonza aje hadharani aseme kikao chake na Mwigulu Dodoma kilimhusisha yeye na nani wengine? Anadhani watanzania wote hawajui? Tunamjibu kwa staha bado ila akitaka tuweke hadharani yote tutaweka tuone atakimbizia wapi uso. Yeye anyamaze aende CCM, inatosha, au chama kiingine. Huku anatapatapa tu.

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

Share this :

Related Posts

0 Comments