Wanabidii,
Kuna kitu kimekuwa kikinisumbua moyoni. Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi kuhusu viongozi wetu (waliopo madarakani na wastaafu) na Katika mpya. Kabla Rais hajakubali kuundwa kwa Katiba mpya kila aliyekuwa anaulizwa (ukitoa upande wa vyama vya upinzani) alikuwa anajibu: "Katiba iliyopo inakidhi mahitaji ya sasa - hakuna haja ya katiba mpya". Leo wanapoonana na Tume ya Waryoba ya Katiba, wale wale waliosema Katiba ya sasa inakidhi mahitaji ya sasa, wanatoa mawazo mengi sana mapya yenye kuikosoa Katiba yetu ya sasa. Je, huu si unafiki? Kama si unafiki ni nini? Ama ndio kwenda na wakati?
Magafu
NB: Nasubiri hususani maoni ya Mh Kombani (kama bado hayajayatoa). Bila shaka ataendelea kusema: "inakidhi mahitjai ya sasa - hakuna haja ya katiba mpya".
-- Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 Comments