[wanabidii] WANAHITAJIKA WALIMU WA KISWAHILI

Wednesday, November 07, 2012

Napenda kukaribisha maombi ya watu mbalimbali wanaoweza kufundisha Kiswahili kwa muda wao wa ziada haswa siku za mwisho wa wiki na jioni kwa njia ya mtandao .


Tumeingiza rasmi lugha ya Kiswahili kwenye mawasiliano ya mradi huu kwahiyo tunataka wahusika mbalimbali wajifunze Kiswahili , historia na masuala mbalimbali yanayohusu Kiswahili .


Sifa za Mwalimu :


Awe anajua Lugha ya Kiingereza na Kiswahili akiwa anajua na kifaransa au kiarabu itakuwa vizuri zaidi .


Awe mwelewa na mjuaji wa mitandao ya kijamii kama facebook kwa ajili ya kutoa masomo na kuwasiliana na wanafunzi .


Awe ana jina la Skype na awe na Laptop yenye kamera na sauti nzuri au kifaa cha kuongelea .


Awe anajua tamaduni , maadili na historia ya Kiswahili .


Tabia zako na sifa zako mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii zitaangaliwa unapotuma maombi yako .


Malipo :


Malipo ni Dola 5 kwa saa moja ambayo inabadilishwa kwa hela za nchi ambayo mwalimu yupo . Tunategemea ufundishe masaa 2 au zaidi .


Maombi yatumwe kwa oldmoshi@gmail.com

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

Share this :

Related Posts

0 Comments