[wanabidii] Tashwishi kuhusiana mchakato wa uundaji wa katiba mpya unaondelea.

Monday, November 26, 2012
Kuna kitu sikielewi. Muswada wa marekebisho/ marejeo/ mabadiliko ya katiba ulipopelekwa bungeni kwa mara ya kwanza na serikali, ulipingwa na kukataliwa na wanasiasa, wanaharakati na umma kwa ujumla wake kwa sababu ya lugha na mambo mengine ya MSINGI SANA yaliyokuwa yanashiwishi kuwa kama muswada ule ukipita bila kufanyiwa marekebisho, basi kuna uwezekano mkubwa sana tu katiba ijayo ikawa haina tofauti saaana na hii iliyopo ISIPOKUWA TU kama serikali ya CCM itaamua sasa (kinyume na historia) kuweka mbele maslahi ya taifa ya muda mrefu, na kuacha kuweka mbele maslahi yake ya kisiasa ya muda mfupi katika kipindi hiki ambacho iko madarakani.
Kwahiyo muswada ule ulipingwa vikali na umma, serikali ikaambiwa iutoe muswada ule na ikapewa muda wa kuufanyia marekebisho tajwa. Mwisho wa siku muswada ule ulirudishwa bungeni huku marekebisho pekee yaliyofanywa kwenye muswada huo yakiwa Lugha, vifungu vya msingi zaidi ya lugha vilivyokuwa vinaibaka demokrasia viliachwa bila kufanyiwa marekebisho (mf. kumpa rais mamlaka na madaraka makubwa yaa kuingilia mchakato wa uundaji wa katiba mpya, na kipengele kilicho husu upatikanaji wa wajumbe wa Constitutional Assembly vikiwa vimeachwa bila kubadilishwa hata nukta.)
Muswada uliporudi bungeni kwa maara ya pili ULIPITISHWA KWA NGUVU na bunge bila ridhaa na kinyume cha matakwa ya umma, hatimaye ukawa sheria kamili.
Sasa hivi umefika wakati wa tume kukusanya maoni, wale waliokuwa wanaukataa ule muswada ndio wanaohimiza watu wakatoe maoni yao kwenye hiyo tume, hii inatoa tafsiri gani??? Ni kitu gani kimeisafisha sheria hii na kuipa uhalali wa kukubalika before the public that rejected it toka ilipokuwa muswada??? sielewi. Kwanini tulipoteza mudaa kutokaa bungeni kupinga upitishaji wa sheria hii??? kwanini tuliandaa makongamano na hata maandamaano kupinga sheria hii halafu sasa hivi tunakubaliana na provisions zake na kuhimizana kwenda kutoa maoni kwenye Tume????

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk
CORE 2 DUO
2.0 GHZ CPU
2 GB RAM
DVD/CD - RW
WINDOWS 7 /WINDOWS XP
WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0718 637905
0786 806028
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

Share this :

Related Posts

0 Comments