maambukizi ya virusi vya Ukimwi kwa kuwa zina vichocheo vingi ambavyo
vinahuisha virusi vya Ukimwi katika nyumba ya uzazi na kuvipa nguvu ya
kusambaa.
Inaelezwa kuwa walio katika hatari zaidi ya maambukizi hayo ni
wanawake walioko katika ndoa kwa kuwa ndiyo wanaotumia zaidi sindano
hizo.
Utafiti huo uliofanywa na wanasayansi wa Marekani na kuripotiwa na
gazeti la The Guardian la Uingereza, umebaini kuwa wanawake wanaotumia
sindano za uzazi wa mpango wapo katika hatari mara mbili ya kupata
maambukizi ya Ukimwi au kuwaambukiza wenzi wao, kuliko wengine.
Katika utafiti huo uliofanywa katika nchi saba zinazoendelea barani
Afrika ikiwamo Tanzania, wanasayansi hao kutoka Chuo Kikuu cha
Washington, walipendekeza ushauri zaidi utolewe kwa wanandoa kabla mtu
hajajiingiza kwenye matumizi ya sindano kama njia ya kupanga uzazi.
Utafiti huo ulifanyika kwa wanandoa 3,790 kutoka nchi za Tanzania,
Afrika Kusini, Zimbabwe, Uganda, Kenya, Rwanda na Botswana,
ulichapishwa kwa mara ya kwanza katika Jarida la Afya la Lancet kabla
ya kunukuliwa na gazeti la The Guardian.
Utafiti umebaini pia kuwa zaidi ya wanawake 140 milioni duniani
wanatumia njia mbalimbali za uzazi wa mpango, huku wanandoa wengi
katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, wanaoishi na VVU
wakichagua kutumia sindano kama njia ya kuzuia mimba zisizotarajiwa.
Wanasayansi hao walikusanya taarifa kati ya wanandoa 3,790 ambao mmoja
wao anaishi na VVU na mwenza wake akiwa hana maambukizo.
Aidha, wanawake ambao wanaishi na VVU na wanatumia sindano hizo pia
walikuwa katika hatari zaidi ya kuwaambukiza wenzi wao.
Vipimo vilionyesha kuwa sindano hizo ambazo zina vichocheo ambavyo
vinavipa nguvu virusi ndani ya nyumba ya uzazi (cervix).
Imeelezwa kuwa njia za uzazi wa mpango zinazohamasishwa zaidi na
kupendwa zaidi na wanawake ni sindano, ambazo wanawake wanasema kuwa
zinadumu kwa muda mrefu na zinaweza kutumika bila ya ruhusa au mume
kufahamu.
Kiongozi mkuu wa utafiti huo, Renee Heffron wa Chuo Kikuu cha
Washington alisema sindano za uzazi wa mpango zina vichocheo vingi
ambavyo huvihuisha vijidudu vya Ukimwi katika nyumba ya uzazi na
kuvipa nguvu ya kusambaa.
"Ni vyema sasa kama tutasisitiza njia za uzazi wa mpango ambazo ni
salama zaidi kama vile mipira ya kiume au njia nyingine ambazo hazina
vichocheo (hormones) au zina kiasi kidogo cha vichocheo," alisema Dk
Heffron.
Mwanasayansi mwingine, Charles Morrison wa Kituo cha Afya cha Durham,
nchini Marekani alisema uhamasishaji wa matumizi ya sindano za uzazi
wa mpango unachochea maambukizi zaidi katika nchi za Jangwa la Sahara.
"Ushauri wangu kwa nchi zinazoendelea ni kuacha matumizi ya njia za
uzazi wa mpango zenye vichocheo, ili tupunguze maambukizi, jibu la
tatizo hili linatakiwa litafutwe sasa, nchi zinazohusika zinatakiwa
zishiriki katika hili," alisema.
Alivitaka vituo vya afya vitoe ushauri kwa wanawake kutumia kondomu
badala ya sindano au vidonge.
Mara nyingi watu wanaotumia vidonge, wengi si wanandoa, mtu anayemeza
vidonge vya kuzuia mimba anaogopa zaidi mimba, si Ukimwi.
Huchoche hamu ya mapenzi
Mfamasia katika Kitengo cha Dawa kwa watu wanaoishina VVU katika
Hospitali ya Amana, Christopher Masika alisema anaafiki kuwa sindano
na hata vidonge vinaweza kuwa ni sababu inayochochea maambukizi kwa
sababu ya uhuru.
"Ninachokiona mimi katika hilo ni uhuru. Mtu anapotumia sindano huwa
huru kufanya ngono kwa kuwa hana hofu ya mimba, hicho kinaweza
kumfanya apate maambukizi kwa urahisi, tofauti na anapotumia kondomu,"
alisema.
Alisema wapo baadhi ambao wakitumia sindano hizo vichocheo vinawafanya
wapate hamu zaidi ya kufanya mapenzi, hivyo huanza kutembea na wanaume
wengine.
Aliongeza kuwa mtu anayeishi na VVU akizuia mimba kwa njia ya sindano,
ni rahisi kupata maambukizi mapya kutoka kwa mwenza wake.
Masika alisema wanawake wapewe elimu zaidi kwani wapo ambao
wanadanganywa kuwa njia za uzazi wa mpango kama sindano, povu zinaweza
kuzuia maambukizi, jambo ambalo si la kweli.
Wakati huohuo baadhi ya wanandoa wanaoishi na VVU wanaopata matibabu
katika Hospitali ya Amana wamesema kuwa tangu waanze kutumia dawa za
kupunguza makali ya Ukimwi (ARVs) hamu ya kufanya mapenzi imeongezeka
kwa kasi kubwa.
Mkuu wa Kitengo cha Utafiti cha Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi
(Tacaids), Dk Arodia Mulokozi, alisema taasisi yake haiwezi kuzungumza
lolote kuhusu utafiti huo, badala yake alilitaka Mwananchi kuzungumza
na Kitengo cha Afya ya Uzazi wa Mpango cha Muhimbili.
"Hatuhusiki na masuala ya uzazi wa mpango, nafikiri unaweza kuzungumza
na Kitengo cha 'Reproductive Health' cha Muhimbili," alisema Dk
Mulokozi.
Waziri wa Afya hakupatika, lakini msemaji wa wizara hiyo, Nsachris
Mwamwaja alisema ni mapema mno kuchangia kuhusu utafiti huo, atafanya
hivyo pindi atakapopata taarifa zaidi.
Mratibu wa Mpango wa Uzazi wa Mpango Tanzania (Umati), Dk Morris Hiza
amekiri kuufahamu utafiti huo, lakini akaeleza kuwa haujajitosheleza
na bado una maswali mengi.
"Nilikuwapo wakati Heffron anawasilisha utafiti wake mjini Geneva,
lakini nakumbuka mkutano ule wa WHO (Shirika la Afya Duniani)
uliukataa," alisema.
Alieleza kuwa Heffton alifanya utafiti huo kwa nyani na wanawake
makahaba pekee.
http://www.mwananchi.co.tz/habari/-/1597578/1625530/-/vhqmiq/-/index.html
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
DELL LATITUDE D 620 & D30
80 GB HardDisk
CORE 2 DUO
2.0 GHZ CPU
2 GB RAM
DVD/CD - RW
WINDOWS 7 /WINDOWS XP
WIRELESS , BLUE TOOTH .
TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY
CALL : 0718 637905
0786 806028
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 Comments