[wanabidii] MFUMO WA ELIMU NA AJIRA JE UNAWEZA KUTOA VIONGOZI NA WATUMISHI WAADFILIFU

Friday, November 09, 2012
Wanabidii,
Nimekuwa mara nyingi najaribu kufuatilia mijadala mingi inayotolewa hapa jukwaani na wakati mwingine katika sehemu nyingine katika majukwaa ya kijamii. Nimeona mara znyingi na kama si zote hoja ikitolewa michango yake huwa ni malalamiko na  mwisho huwa ni kukata tamaa.
 
Ambalo nimekuwa pia nalishuhudia ni malalamiko jinsi elimu yetu na mfumo mzima wa ajira usivyoweza kutoa watumishi wenye uadilifu unaweza kulipeleka taifa hili mbele. Yawezekana hoja hii ilikwisha kujadiliwa kama ni hivyo naomba nijulishwe na hoja ifungwe, la si hivyo basi naomba hebu tujielekeze kwenue hoja yenyewe kwamba JE MFUMO WA UTOAJI WA ELIMU NA MFUMO WA AJIRA YETU HAPA NCHINI UNAWEZA KUTOA VIONGOZI NA WATUMISHI WAADILIFU? ninacholenga ni uchambuzi wa kina wa mfumo wa utoaji wa elimu na elimu yenyewe jinsi inavyomuandaa mtoto hadi kijana kuitumikia nchi yake, yapi mapungufu yake kisha nini kifanyike kuondoa mapungufu haya.
 
Aidha nalenga pia kuwe na uchambuzi wa kutosha juu ya mifumo iliyopo ya Ajira nchini, yapi mapungufu yake na nini kinaweza kufanyika ili kurekebisha kasoro au kuondokana kabisa na mifumo hii kama haifai.
 
Uzoefu wangu hapa unaniaminisha kuwa hoja hii itachangiwa na kisha kupata mwafaka wake. Karibuni TUJADILIANE.
 
K.E.M.S.

Share this :

Related Posts

0 Comments