[wanabidii] MALIPO YA MAFUTA NA GESI YA ZNZ NI: VYARAHANI NA NG'OMBE KUTOKA UARABUNI!

Tuesday, November 06, 2012
Shemeji Issa,
Hii ya leo ni babu kubwa!!!
Nami naomba charahani kimoja mkeshaanza kupata hayo mafuta!
Ugomvi wote ule wa nini? Kumbe shida yenyewe ni kupata vyarahani na ng'ombe tu?
Zilizobakia wanaume wazipeleke Uswiss!
Huu ndio umaskini wetu Waafrika - hatufikiri. Eti kubwa ni kutapa vyarahani na ng'ombe!
Mkeshapata vitu hivyo mtakuwa ni wenye maendeleo na furaha!
Ras Gas watakuibieni tu hayo mafuta na gesi yenu kama kweli mnayo. Rasul Khaimah yenyewe ni taabani na kila siku inaomba Dubai na Abdu Dhabi.
At the end of the day, ninaona mtabakia kuja kusota huku huku Kariakoo - lakini Mzee Makundi hatokuruhusuni tena wakati huo!
Mnataka kuuvunja Muungano kwasababu ya kupata vyarahani na ng'ombe tu!!! Ninacheka sana leo.
Anyway, kila la kheri shemeji, lakini usije kunisahau na hicho charahani kimoja kwaajili ya dada yako - fanya viwili na mpwao kimoja!


//Nkumba.

Share this :

Related Posts

0 Comments