Eti sasa nauli ya ndege Mwanza Dar ni elfu 32! yaani hata ile mikweche ya mabasi haifikii! Ila sasa sambusa na chai inabidi ujilipie! mpaka sasa booking za november zimejaa kumbe watu wanaupenda huu usafiri asikwambie mtu. Ila vile viroba vya sato sangala na mchele itabidi vilipiwe na wale wabwana mkubwa wa business class wao ka bei kako palepale. Sasa ile adha ya kuchuchumalishwa kwenye korido marcopolo linapofika mizani itakwisha. Naamini hawa jamaa ni sustanable sio wale wa ndege ya jamii manake watasha wenyewe wanasimamia.
Mzee shirima yeye amesema atakula chocho ambazo hawa watasha hawawezi kufika shughuli hawa waswahili! nasikia wameshusha bei lakini hizo tenda za mapochopocho bado wanatubebesha! akha mie ntaenda na ugali wa lowe bora nisafiri kwa bei nafuu.
-- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 Comments