na majibu kwa muda mrefu, huku kukiwa na nyimbo tele kuwa bei
itakuwa nzuri mwaka huu au mwakani ule , mwaka ujao huku
misimu ya zao hilo ikisonga mbele bila ya kuwa na majibu.
Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi juu ya bei ya zao hili ambalo kwa
hakika limekuwa mkombozi wa wakulima wengi huko mikoa ya kusini mwa
Tanzania hasa Mtwara. Mafanikio hayo si ya kusimuliwa kama hadithi
ya adili na ndugeze tu bali mengine ni ya kuona kwa macho yangu kwa
wale wakulima wa korosho ambao nina nasaba nao huko Mtwara
Kwa desturi ya majira ya Mkoa wa Pwani mara zote korosho zake
uanza kuokotwa mwishoni mwa mwezi wa10 uokotaji huo uongezeka na
kumalizika mwezi wa 12 nako huko Mtwara wenzetu wakiokota korosho
hizo kuanzia mwishoni mwa mwezi wa tisa na mwezi wa kumi
msimu unakuwa umepamba moto kweli kweli mwezi wa kumi na moja kazi
ya kuokota huwa imemalizika.
Tafauti ya vipindi hivyo ina manufaa makubwa kibiashara kuwa wakati
Mtwara wanamaliza kuokota tambua kuwa Pwani korosho zinaanza
kwa hiyo kila mmoja anaweza kuwa nafasi ya soko la bidhaa yake,
iwe rejareja, jumla , nchini au nje ya nchi yetu.
Cha kusikitisha wakati Mtwara wakisonga mbele kwa kuwa na bei
bora Pwani hali imekuwa hoehae. Kwa kwa sasa yani Novemba 2012
bei yake ni shilingi mia 300 ikizidi basi ni 400. Wakati Mtwara
wanaweza kuuza Korosho zao hadi kilo 2000 Je Mkoa wa Pwani
unashindwa kwa nini? Au Wilaya ya Mkuranga inashindwa kufanya hivyo
kwa sababu zipi? Je watawala hawapendi kuiona …,Je kwanini
wapende kuiona meli ya Mtwara baharini na wasipende kuiona meli
ya Pwani baharini?
Hapo awali kulikuwa na madai kuwa vyama vya ushirika vitaweza
kuwakomboa wakulima wa Korosho kwa ununuzi wa stakabadhi ghalani
lakini mpaka sasa Wilayani Mkuranga stakabadhi ghalani imekuwa
kero huku wakulima wengi wakiwa na kilio cha kutopokea fedha zao
za awamu zilizopita. Kuna madai kuwa baadhi ya watendaji wa mfumo
huo wakinunua zao hilo wakijipatia wenyewe malipo hayo.
"Hali ya sasa inatuvunja moyo mathalani kupalilia heka moja ni
elfu sitini kuimwagia dawa mikorosho ni elfu arobaini, Je hiyo
kilo ya shilingi 300 itanisaidia nini."anasema mama mmoja mwenye
Umri wa makamo Kijini Kiziko Wilayani Mkuranga, Mkoani Pwani.
Hali ya kukatishwa tamaa ya mkulima huyo inathibitishwa na mandhari
ya maeneo mengi ya Wilaya hii kwa kuona Mikorosho mingi ikiwa
imekatwa hovyo wengine wakiikata na kuchoma mkaa huku wengine
wakisema kuwa tunafanya hivyo angalau tupande miembe ya muda
mfupi kwa kuna sasa embe zina soko.
Je pengine Wilaya ya Mkuranga imekosa mtetezi wa zao hilo? Bila ya
kuuma maneno inawezekana kuwa imekosa mtetezi wa zao hilo japokuwa
Naibu Waziri wa Kilimo Adam Malima Mtoto wa Marehemu Profesa Kigoma
Ally Malima Mzaliwa wa Mkamba kuwa ndiye Mbunge wa jimbo hilo.
Je ni kweli Adam Malima ataweza kusaidia wakulima wa mazao mengine
ya biashara kuwa na bei bora wakati wakulima wa Korosho zao la
biashara jimboni kwake wakiwa hoi bin taabani wakitafuta pa
kushikilia. Jawabu ya swali hilo naamini unalo wewe msomaji wa
makala haya ya zao la Korosho Mkoani Pwani.
Kw a hakika kumekuwa na juhudi za kutatua kero hiyo ya bei ya zao
hi li kutoka Ofisi ya Mkoa w Pwani Chini ya Usimamizi wa Bi
Mwantumu Mahiza ambaye ndiye Mkuu wa Mkoa wa Pwani kwa kutoa
ahadi ya kywashungulikia wale walisheka kibindoni pesa za wakulima
waliouza korosho kw a stakabadhi ghalani. Lakini juhudi hizo
zinakuja wakati mbaya kwani msimu wa zao hilo umeanza huku wakulima
hao hawana pesa za msimu uliuopita ambazo zinginunua dawa na
kutumika kupalilia Mikorosho hiyo.
Malalamiko ya wakulima wa zao hilo ni mengi si kukwapuliwa
kwa pesa zao za stakabadhi ghalani tu bali kumekuwa na tabia ya
wale wanaonunua korosho kwa stakabadhi wamekuwa wakinunua korosho kw
a wakulima kwa njia ya kawaida baadae wanauza wao kwenye
stakabadhi ghalani ili malipo yakija basi wao wanapewa pesa
hizo.
Juu ya bei ya zao la Korosho na Ubunge wa jimbo la Mkuranga
vimemzidi kimo ndugu Adam Malima naamini analo mwenyewe
Mheshimiwa Malima.
Kwa hakika wale tulibahatika kumuona Profesa Kigoma Malima baba
Mzazi wa Adam Malima tunajua kuwa alikuwa na juhudi na nia njema
kwa wakazi wa Mkuranga hasa akisisitiza umuhimu wa elimu wakati
huo ambapo Wilaya ya Kisarawe ikiwa nyuma kielimu.
Binafsi siafiki kabisa wakazi wa Mkuranga kukata mikorosho na
kuchoma mkaa bali ni jukumu la wapanga sera kuweka utaratibu
sahihi wa bei ya zao hili ambalo kwa hakika linawezekana kuwa
na bei ya kutosha ambayo mkulima atanufaika na serikali pia.
Kama itaonekana imeshindikana basi wanunuzi wa rejareja waruhusiwe
kununua na kusaidia kuwapa nafasi wakulima kuweza kuuza kwa bei
bora iwe Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani au ata huko Mtwara
kwenye bei bora.
Wasalaam Adeladius Makwega
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 Comments