[wanabidii] Zitto Apeleka Hoja Bungeni Kutaka Uchunguzi Walioficha Mabilioni Nje - Mwanzo

Thursday, October 04, 2012

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ameiandikia barua Ofisi ya Bunge kuitaarifu nia yake ya kuwasilisha hoja binafsi katika Mkutano wa 11 wa Bunge kuliomba liazimie Serikali iwasiliane na taasisi za kimataifa, hasa benki kusaidia kurejeshwa nchini fedha zote haramu ambazo zimefichwa na Watanzania katika benki za nchini Switzerland na kwingineko duniani.

Taarifa zilizopatikana jana kutoka Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni zimeeleza kuwa Zitto anaomba Serikali ifanye hivyo kwa Benki ya Dunia kupitia taasisi yake ya Stolen Asset Recovery Initiative, kutekeleza jukumu hilo. Taarifa hizo zimeeleza kuwa katika barua hiyo Zitto anatumia kifungu cha kanuni za bunge namba 55 (1) na (2), na hoja yake itaainisha fedha ambazo Benki ya Taifa ya Switzerland ilitangaza kwamba Watanzania wamezihifadhi, ambazo ni Sh297 bilioni.


http://wotepamoja.com/archives/8031#.UG0uML28MqA.gmail

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

Share this :

Related Posts

0 Comments