Kuna msemo maalufu usemao "usipo jiajiri shetani anakuajiri"! Naashawishika kusema kuwa ndugu zetu waliotoa tamko hili na wale wote wanaowashabikia wameshindwa kujiajiri na sasa shetani amewaajiri... bahati mbaya ajira ya shetani ni katika mambo ya kishetani. kama vile kuharibu mali za watu, kuchoma makanisa, kukurupuka hata pasipostahili kufanya hivyo, kuendesha mihadhara ya kukashifu wengine badala ya kuhimizana kufanya kazi, kukosa wivu wa maendeleo, kuchukia maendeleo ya jirani yako, kuchukia elimu dunia, kutotambua mchango wa wengine kwako, kulalamika sana hasa pale usipoonewa, kusema uongo, kukimbilia kuvuna usipopanda, kutaka uhurumiwe n.k.
Kuvalia njuga suala la mtoto emmanuel asiyejua kuwa Qur'an ni takatifu ni ajira ya shetani. kama si hivyo basi yule mtoto wa kiislam aliyeleta kitabu kitakatifu wakaanza kukichezea ndiye wa kuadhibiwa maana anajua kile si kitabu kama vingine. kwa Emmanuel Qur'an ni sawa na vitabu vingine kwani kwake kitabu kitakatifu ni Biblia. kumlazimisha akione ni kitakatifu ni kumsilimisha kwa nguvu. Hivyo hata kumshikilia mtoto Emmanuel polisi ni uonevu. akili ya kawaida (common sense) inakuonesha kuwa adhabu wanayotaka itolewe kwa mtoto emmanuel ni kubwa mno.
Mzazi gani anayekuta watoto wawili wanachezea chakula alichotengewa baba akamuadhibu mmoja tena yule wa jirani asiyejua kuwa kilikuwa chakula cha baba mwenye nyumba?? ni uonevu tu.
Kuchoma makanisa ni ajira ya shetani. kuna uhusiano gani kati ya kosa la mtoto Emmanuel na mwenzake na kuchoma makanisa? ebu kuweni wakweli hawa si wahuni!!! maana mtu mwenye kazi hataacha shughuli zake akakimbilia kuchoma makanisa, kuharibu magari...
Nyie Wanajumuia ya Kiislamu ebu acha kujidharirisha kwa kuvalia njuga jambo lisilokuwepo. Mnataka serikali itamke nini?? nachelea kusema kuwa kuna siku wake zenu watagoma kuwapikia then mtaiomba serikali itoe tamko.... sitaki kuamini kuwa na nyie mlikuwa kati ya wale waliochoma makanisa, kufunga barabara na kuharibu mali!!!! wasaidie vijana wetu wayaone maisha ya dunia kuwa nayo ni bora kwao.
Ushauri: Ebu nguvu mnayowekeza katika mihadhara ya kukashifu, kuchoma makanisa, kulalamika, matamko ya kuomba muonewe huruma ielekeze katika yafuatayo:
- kujenga shule nyingi na bora kwa vijana wenu
- kujenga vyuo vikuu na vya kati kwa vijana wenu
- kuwekeza katika miradi ya maendeleo n.k
Mkijikita huko hamtagombania ajira za shetani tena.
Mwisho: Wale waliotaka kumuua mtoto Emmanuel wafunguliwe kesi ya mauaji.
Taasisi na Jumuiya za Kiislamu nchini Tanzania wametoa tamko kufuatia kitendo cha kijana Emmanuel Josefati (14) kukojelea kitabu kitukufu cha Qur'an na kusababisha mgongano wa mawazo miongoni mwa watanzania.
Katika tamko lao wamesema 'Tunalaani Kitendo cha kukojolewa Qur'an Tukufu ambayo ni Kitabu Kitakatifu kwa Waislam Wote Duniani'.
'Tunataka kusikia tamko la serikali la kulaani kitendo cha kukojolewa Qur'an'.
0 Comments