NINESOMA RIPOTI YA KAMATI YA NCHIMBI KUSIANA NA KIFO CHA MWANGOSI. SINA SHIDA NA UDHAIFU WA HADIDU ZA REJEA ZA NCHIMBI KWANI NDIYO YALIKUWA MATAKWA YAKE JAPO UKISOMA UTANGULIZI WA RIPOTI UTAONA HAUTAFSIRIWI KATIKA HADIDU ZA REJEA. SIJUI NI UKOSEFU WA WELEDI KATIKA KUFANYA RESEARCH KWANI KWA KUWA HOJA KUBWA NI KUUAWA KWA MWANGOSI MIKONONI MWA POLISI NILITEGEMEA UCHUNGUZI WA KINA KUHUSU MAZINGIRA YA KUUAWA NA SIO BLABLA ZA KISIASA.
- SEHEMU KUBWA YA TAARIFA IMEJAA UTETEZI BADALA YA UCHUNGUZI HURU WA PANDE ZOTE
- KUNA MALALAMISHI MENGI DHIDI YA CHADEMA NA UTETEZI KWA POLISI
- HAIELEWEKI PICHA YENYE ASKARI POLISI SABA ILIYOONESHWA UKURASA WA 10 INATHIBITISHA HOJA GANI KATIKA TAARIFA WAKATI TAARIFA HIYO INAHITIMISHA KWA KUSEMA KUWA NGUVU YA POLISI ILIYOTUMIKA ILIKUWA SAHIHI NA KUWA MAUAJI HAYAKUPANGWA
- MTU YEYOTE MWENYE AKILI ANAJIULIZA KUMSHAMBULIA MWANGOSI NA KUMUUA KULIKUWA KUNAISAIDIAJE SENSA AU NDIKO KULIKOVURUGA ZAIDI
- MAPENDEKEZO YA KAMATI NI DHAIFU KWANI HAYAONESHI KUEPUKANA NA VURUGU WALA KUTOUAWA KWA MWANDISHI WA HABARI, RAIA WATII SHERIA SAWA LAKINI POLISI JE?, NI NINI MAANA YA ULINZI SHIRIKISHI KATIKA SUALA HILI?, WAANDISHI KUWA NA MAVAZI RASMI NI KICHEKESHO KWANI MWANGOSI HAKUUAWA KWA SABABU YA KUTOKUWA NA MAVAZI NA YANAWEZA KUWAHATARISHA ZAIDI KWA POLISI WENYE UDHAIFU KATIKA KUFANYA KAZI ZAO
|
|
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
Share this :
0 Comments