[wanabidii] Mtoto Adhalilishwa Msibani kwa Barlow - Mwanzo

Tuesday, October 16, 2012

WAKATI vilio, simanzi na huzuni jana vikighubika jiji la Mwanza wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Liberatus Barlow, mwanafunzi wa darasa la tano amedhalilishwa kingono na mtu asiyefahamika.

Mbali ya simanzi hizo, baadhi ya waombolezaji walianguka na kuzirai akiwemo mkewe, Marystella Barlow, aliyeishiwa nguvu ghafla katika tukio hilo ambalo lilihudhuriwa na mamia ya watu wakiwemo viongozi wakiongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi.

Pia makamanda wa polisi wa mikoa yote sita ya Kanda ya Ziwa, walishiriki shughuli hiyo iliyofanyika katika Uwanja wa Nyamagana na baadaye jioni mwili kusafirishwa kwa ndege kwenda jijini Dar es Salaam ambapo familia ya marehemu inaishi.

Katika hatua ya kushangaza, mwanafunzi huyo wa shule moja jijini hapa, alijikuta akifanyiwa udhalilishaji wa kingono kwenye maungo yake sehemu ya makalio ambapo mwanaume mmoja asiyefahamika alimchafua sare yake kwa kumwagia manii pasipo kujua.


http://wotepamoja.com/archives/8848#.UHzmJzoR7TY.gmail

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

Share this :

Related Posts

0 Comments