[wanabidii] Dk Shein atangaza vita na wavunjifu wa amani Zanzibar

Friday, October 26, 2012
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa ustahamilivu na uvumilivu wa Serikali umefikia kikomo kwa wale wote wanaofanya vitendo vya fujo na vurugu na itamshughulikia ipasavyo mtu yo yote atakaevunja sheria. Dk. Shein aliyasema hayo leo katika hotuba yake aliyoitoa kwenye Baraza la Idd el Hajj.Lililofanyika huko katika hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar.Katika hotuba yake hiyo Dk. Shein alisema kuwa ustahamilivu na utulivu sio udhaifu ni heshima kubwa ya kutii amri ya Mwenyezi Mungu na kusisitiza kuwa hatua ya serikali kuvumilia vitendo hivyo vya uvunjifu wa amani sasa basi. "enough is enough", alisisitiza Dk. Shein.

Share this :

Related Posts

0 Comments