Ndugu wanabidii, Kama mlivyosikia na kuona kwenye vyombo vya habari, mama mmoja katika wilaya ya Kibondo huko Kigoma, amevamiwa usiku na askari polisi wanne, wakampiga sana na kumnyang'anya shilingi milioni mbili na simu zake nne! Kwasa mama huyo amelazwa hospitali ya wilaya kutokana na kipigo hicho na askari wamekamatwa na kuwekwa selo. Matukio ya aina hii ni mengi mkoani Kigoma yakiwamo ya vitisho na kubambizwa kesi! Nawaomba wanaharakati, wanasheria, wanahabari pamoja na wadau wengine mfuatilie suala hili ili haki itendeke. La sivyo, polisi hao wataachiwa bila hata ya uchunguzi wowote! Nawasilisha; Mwl.Mbanyi |
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 Comments