Uhalifu wa Mitandao – Mifano ya Tanzania
Watu wengi wamewahi kusikia uhalifu haswa wizi wa mitandao kwa simulizi au hata pale unapowatokea wanakua hawajui cha kufanya au hata kujua tu kwamba kitendo hicho ni uhalifu wa mtandao .
Uhalifu wa Mtandao ni nini ?
Ni uhalifu wowote unaohusisha vifaa vya mawasiliano katika kutekeleza uhalifu husika , vifaa kama simu za mikono , moderm , computer , ipads na vingine vinavyosaidia kurusha mawasiliano hayo toka sehemu moja kwenda nyingine .
Kwa Tanzania kuna mifano kadhaa ya uhalifu wa aina hii , haswa unaohusisha taasisi za fedha zaidi benki na kampuni za simu za mikono .
WIZI WA BIL 2.3
Uhalifu huu umetokea miezi 2 iliyopita , ambapo watu karibu 10 walihusika lakini wengi wao wakiwa ndani ya kampuni hiyo ya simu .
Kilichofanyika .
Wafanyakazi hawa walitafuta akaunti ya mfanyakazi mwingine aliyeacha kazi na kufanikiwa kupata namba zake za siri , wakaingia na kutengeneza mawakala bandia wa huduma za fedha .
Baadaye mawakala hawa walipewa fedha hizo na wao kuzitoa kwa njia ya kuhamisha kwenda kwenye benki mbalimbali na watu wengine mbalimbali mpaka kufikia kiasi hicho cha fedha .
Je Benki haikushituka ?
Inasemekana benki ilishtuka baada ya kuona kiasi kikubwa cha pesa kinahamishwa kilichofikia mil 400 hivi , walipopiga simu kwenye kampuni husika ni wahalifu wale wale waliopokea na kuidhinisha fedha hizo kuhamishwa .
KUPOTEZA /KUIBIWA LAINI AU NAMBA ZA SIMU
Kuna watu wengi wanaibiwa , kupoteza laini za simu zenye hela au hata Kusahau na wanakaa muda mrefu bila kutumia au hata kuangalia vitu kama salio na taarifa nyingine kuhusu laini zao kama ni sahihi au la .
Kama laini yako imepoteza mawasiliano inawezekana ni mtu ameiba namba hiyo kwa kupiga kwenye mtandao wa simu na kutoa taarifa zako kama vile ndio wewe , kwenye mtandao wa simu watamtengenezea namba kama yako na ataweza kuitumia kama ulikuwa na fedha ataweza kuhamisha fedha hizo kama ni uhalifu anaweza kufanyia pia .
Kama unapigiwa na mtu ambaye humjui anayejifanya ni mfanyakazi wa mtandao wako wa simu , uwe makini anaweza kuwa anataka kufanya uhalifu pale utakapompa taarifa zako ambazo ni sahihi .
Watu wengi wanatumia miaka yao ya kuzaliwa kama neno la siri yaani PWD , unatakiwa kubadili hili ni rahisi mtu kuhisi na kukufanyia maajabu .
UTUMIAJI WA SIMU BANDIA / AMBAZO HAZINA VIWANGO
Nchini India serikali ya nchi hiyo imepiga marufuku utumiaji wa simu bandia maarufu kama mchina , nchini kenya taasisi ya mawasiliano ya nchi hiyo inaelimisha wananchi sana kuhusu umuhimu wa kutumia simu original , genuine na mpya .
Nini Hutokea ?
Simu zote huwa zinatambulika na namba fulani maalumu kwa ajili ya mawasiliano na huduma nyingine , ukiacha namba ya simu ambayo unaweza kubadili mara kwa mara .
Unapokuwa na simu bandia namba hizo zinaweza zisiwepo au zinaweza kuwa zinafanana na mwingine ambaye anaweza kuwa mhalifu , lakini zaidi ni kutoonekana kwa simu hiyo endapo kumetokea uhalifu au hujuma nyingine .
Simu hizi hazijatengenezwa kwa viwango vinavyokubalika kimataifa kwa ajili ya mawasiliano , kwahiyo unapotumia kuna uwezekano mkubwa wa kusababisha magonjwa kama saratani , kichwa , ngozi na matatizo mengine mbalimbali .
Ku Flash Simu Je ?
Kuna watu wengi sana wana flash simu zao ili ziweze kusoma laini za mitandao wanayoitumia wao au iweze kupata huduma fulani kutoka kwenye mitandao ya simu .
Kitendo hiki ni kosa kisheria na utaweza kuingia matatani , endapo itathibitika kwamba kuna taarifa za simu zilizoingizwa ambazo sio sahihi kutokana na kitendo hicho cha kuflash simu .
Maana yake umebadili mfumo wa simu hiyo kutoka vile ilivyotengenezwa awali .
ITAENDELEA .
Yona F Maro
9/28/2012 7:17 PM
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 Comments