Ndugu waandishi wa habari
Hivi karibuni kwa zaidin ya mwezi na nusu sasa,kumejitokeza vijana
wanaopita kwenye maeneo mbalimbali katika mji wa Arusha,wakitukana na
kukikashifu chama chetu cha CHADEMA,matusi na kashfa hizi ni matokeo
ya ripoti ambayo iliandaliwa na vijana watano wasomi wa chuo
kikuu,waliotumwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bwana Malongo
Magesa.Itakumbukwa kuwa Mkuu huyu wa mkoa wa Arusha aliletwa Arusha
kwa sababu maalum,na moja ya sababu hizo ni kukidhoofisha
CHADEMA,hivyo aliunda kikosi kazi hicho ambacho hata hivyo miongoni
mwa vijana hao watano watatu ni vijana wangu,walizunguka Arusha,na
kumletea ripoti MBOVU ambayo kwa UPOFU wake naye ameifanyia kazi,moja
ya ushauri waliompa ni kuwatumia wanachama wa CHADEMA kuwatukana
Viongozi wao na chama,hivyo Mkuu wa mkoa pamoja na Meya Feki wa
Kichina,wakawarubuni vijana wawili wanachama wa CHADEMA ambao ni Niko
na Kiyeuyeu.Vijana hawa Niko Na Kiyeuyeu ambao wanalipwa na Mkuu wa
Mkoa pamoja na Meya wa Kichina,wamepewa pikipiki pamoja na Tshs 20,000
kila siku kwa kazi hiyo ya siasa chafu.Tunatoa Rai wa wakazi wote wa
Arusha kuwapuuza Vijana hawa ambao njaa zinawasumbua hadi kufikia
kujisaliti wenyewe.
BAVICHA mkoa wa Arusha tunalaani aina hii ya siasa,na tunamtaka mkuu
wa Mkoa aache kutumia ofisi ya umma kwa maslahi ya ccm vinginevyo
aachie ofisi ya Umma.Tunatambua kuwa mkuu wa Mkoa ana majukumu yake
lakini Bwana Malongo Magesa amekuwa akiingilia utendaji wa
Halimashauri ya manispaa ya Arusha,na kuwa kama Mkurugenzi,hivi
karibuni alizuia Tenda ya kukusanya ushuru wa Mabango,kwa kuwa mzabuni
aliyeshinda sio chaguo lake na badala yake akataka kampuni ya ndugu
yake ndio ipewe Tenda wakati imetender kwa hela ndogo zaidi.
Tangu ateuliwe kushika wadhifa huu huyu RC amekuwa Kituko hapa
Arusha,ameunda zaidi ya Tume tatu kuchunguza ubadhirifu ulio wazi wa
Halmashauri ya manispaa ya Arusha,na hakuna hatua yoyote
iliyochukuliwa huku tume hizo zikiwa zimetumia mamilioni ya walipa
kodi maskini wa Arusha
BAVICHA tunamtaka afanye yafuatayo
1.Aache mara moja kutukana CHADEMA,na Viongozi wake,vinginevyo
tutatangaza mgogoro naye
2.Aeleze umma wa Arusha juu ya Ripoti tatu za tume alizounda za
kuchunguza ubadhirifu mkubwa katika Halimashauri ya manispaa ya
Arusha,aeleze hatua gani alichukua
3.Achague kuwa Mkuu wa mkoa au Mkurugenzi
4.
……………………..
Nanyaro Ephata
Mwenyekiti BAVICHA mkoa wa Arusha
14/9/2012
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 Comments