[wanabidii] Mtanzania mwenye mabilioni ardhini

Saturday, September 29, 2012
Huyu mzee, Dkt. Jumanne Ngoma, yule mgunduzi wa vito vya thamani vya tanzanite mwaka 1967 ambavyo vinawapa utajiri mkubwa watu wa mataifa mengine na kutuacha Watanzania tukizama kwenye umaskini wa kutupwa, kumbe ana eneo lake tangu mwaka 1996 lakini hana uwezo wa kuchimba na wamebaki vijana wake kufukuafukua tu. Hii ni familia tajiri ya ajabu na kama tungekuwa tunajali haki za wagunduzi, huyu mzee angekuwa kwenye orodha ya matajiri barani Afrika.
 
Hii nchi ni kama tumelaaniwa na wiki Mkenya mmoja, Gitau, ametutukana vibaya kwenye TV huko London.
 
http://www.youtube.com/watch?v=WNWAVYF9dEc&feature=relmfu
 
Maskini nchi yetu Tanzania - sijui tuanzie wapi?
 
Matinyi.

Share this :

Related Posts

0 Comments