Edson Kamukara amakuwa akiandika makala yanayoegemea upande mmoja kuhusu mgogoro kati ya jamii za Batemi (Wasonjo) na Maasai (Loita). Hata hivyo editorial (maoni ya mhariri) katika gazeti la leo yamenstusha sana. Nasema nimshtuka sana maana naliheshimu sana gazeti la Tanzania Daima ninalolisoma kila siku.
Awali ya yote naomba nianze kwa kuomba radhi kwa picha nilizoambatanisha (attached) katika ujumbe huu. Gazeti lako linaheshima sana kwa watanzania waliowengi hususan wapenda mabadiliko na wanyonge. Hata hivyo hivi karibuni umechapisha habari kuhusu mgogoro Loliondo katika Wilaya ya Ngorongoro baina ya jamii za Batemi (hatupendi kuitwa Wasonjo) na Wamaasai (kabila dogo la Loita). Habari hizo ambazo zimekuwa zikitolewa na mwandishi wa gazeti lako, jina lipo katika habari hizo, zimekuwa za upande mmoja jambo litakalo tufanya kuangalia gazeti kama la kibaguzi ama waandishi wake wamenunuliwa na upande huo unaopendelewa. Tazama picha za marehemu waliochinjwa kinyama na Wasonjo takroiban mwaka mmoja uliopita na mmoja wa vijana waliopigwa risasi katika tukio la uvamizi lililofanywa na Wasonjo usiku katika Kijiji cha Naan.
Ufuatao ni ufafanuzi baadhi ya hoja za Edson Kamukara katiaka gazeti lako ambazo ni dhahiri zinapendelea upande mmoja kwenye mgogoro huu.
1. Suala la silaha, gazeti lako ikiwepo tahariri yako ya leo tarehe 20/9/2012 zinaonyesha kuwa kitendo na hatua iliyochukuliwa na Serikali kuwanyang'anya Wasonjo silaha ni suala unalolikataa; kwamba lisiwe la nguvu. Unapaswa kufahamu kuwa Wamasai wanachekwa na kuzomewa kwa kupigwa na Wasonjo kwa kuwa walifahamika kihistoria kuwa ni wakali. Jambo la Wamasai kushindwa kujibu mashambulizi ya Wasonjo ni kutokana na kunyang'anywa silaha zote kwani kila mara migogoro inapozuka, Wamasai walikuwa wanaonekana kama wachokozi kwa sababu ya sababu zilizokuwa zikitolewa na Wasonjo kwa Serikali. Hivyo silaha wamekuwa nazo Wasonjo miaka mingi bila kuchukuliwa na Serikali. Kwa hakika tangu Wasonjo wavamie Kijiji cha Wamasai, Naan na kuchukuwa mifugo zaidi ya 2,000 na si 100 kama Kamukara anayodanganya, ni karibu mwezi umepita wanaambiwa wasalimishe silaha na hao mifugo wamekataa. Hivyo tunadhani Serikali imefanya kazi kuchukua hatua kali kuwanyang'anya Wasonjo silaha.
Pili umiliki wa silaha bila kibali ni kosa la jinai ambalo linapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria na mtuhumiwa kunyang'anywa. Hivyo nasikitishwa na mtazamo wenu kuwa eti ifanyike mazungumzo, yawezekana kufanya mazungumzo na wanyang'anyi wa mifugo wanaomili silaha haramu? Serikali haihitaji kujua unapataje silaha unapokuwa tayari unayo na unatumia vibaya, hayo yatakuja baada ya kunyang'anywa silaha, ili usiendelee kutumia kupora mali za watu pamoja kujeruhi ama kuuau. Silaha hizo hizo ambazo gazeti lako linazitukuza, zimetumika kufanyia uhalifu wa kinyama, siku Wasonjo walipovamia Kijiji cha Naan na kuchukua mifugo 2,000 na kujeruhi watu saba pamoja na watoto, na siku waliovamia na kumua mzee wa miaka 90 na kumchoma moto. Siku hiyo pia walishambulia askari walifika katika eneo la tukio jambo lililowapa serikali uhakika kuwa Wasonjo wanamiliki silaha haramu za kivita na posili hawakumuua Msonjo hata mmoja. Huko jiji Dar es Salaam na kwingineko Tanzania tunafahamu kuwa polisi huwaua mara moja majambazi wanaothubutu kuwarushia risasi (Hii isichukuliwe kuwa naunga mkono tabia ya polisi kupiga watuhumiwa achilia mbali kuwaua).
2. Suala la Uraia, eti jamii ya Loita wanatoka nchini Kenya. Madai haya hayana msingi wowote na sii mara ya kwanza kutumiwa na wagandamizaji wa haki za wanyonge kama Wamaasai. Mwanzoni mwa miaka ya 2000 Serikali ya Rais Mkapa ilimnyang'anya urai Mtanzania mzalendo Jenerali Ulimwengu. Kama mzalendo wa viwango vya Jenerali Ulimwengu watadaiwa kuwa ni raia wa kigeni itakuwa Wamaasai wanaopakana na Kenya? Wazalendo wengine kama Zitto Kabwe kwa mfano kuwa tu anatoka mpakani na anawanyima mafisadi usingizi waliwahi kumtuhumu kuwa ati siyo raia wa Tanzania. Wabaya wa Wamaasai kama Kamukara na wengine wengi wanafahamu kuwa siyo Watanzania wengi wanafahamu ukweli kuwa Wamasai wanaishi Tanzania na Kenya; mipaka ya nchi hii iliwekwa na wakoloni na zilipita katikati ya Wamasai hivyo wakawepo Wamaasai wa Tanganyika na Kenya. Hata hivyo, kama kweli kuna Wakenya ndani ya ardhi ya Tanzania je ni nani kawapa Wasonjo jukumu la kuwaondoa?
3. Wamaasai (Loita) na Wasonjo (Batemi) wanapakana, yapo mipaka ya kimila yaliotambuliwa tangu awali lakini leo hii mipaka hiyo haiheshimiwi na ukienda kuangalia bila ubaguzi, wa aina ya Kamukara, utaona huruma kwa Wamasai. Tangu mwaka 1994 wamepoteza ardhi kubwa sana kwani jambo la ajabu limejengeka ambalo halipo katika sheria aina yeyote kwamba, Wasonjo wakilima katika ardhi ya kijiji cha Wamasai mipaka ya Kijiji cha Wamasai itakuwa imeishia hapo kilimo kilipofika. Leo hii kuna maeneo Wasonjo wamelima kuingia katika vijiji vya Wamasai mpaka ndani kabisa na imekuwa kama ndiyo mipaka ya vijiji. Swali langu ni kuwa je mashamba yanasogeza mipaka ya kisheria? Kwamba walipolima Wasonjo ndani ya mipaka ya vijiji vya Wamasai ndiyo unakuwa mwisho wa vijiji vya Wamasai? Yapo maeneo ya Wamasai leo yamekuwa ya Wasonjo kwa sababu tu Wasonjo wanavamia na kulimwa wakati Wamaasai siyo wakulima. Hivyo gazeti lako liangalie lisije likachochea na kuwasha moto kama ule unaowaka kule Tana River nchini Kenya. Katika matukio ambayo picha zake nimekuonyesha wamasai hawakujibu hata moja.
4. Kuhusu eneo ambalo gazeti lako linadai lilisemekana liachwe bila shughuli yeyote; eneo hilo lote limeshalimwa na Wasonjo na hivyo Wasonjo wanachotaka ni Wamasai waondolewe katika makazi yao, ikiwepo Kijiji cha Naan ambacho hata wanafunsi wa Shule ya Msingi Naan hajafanyia mtihani wao katika shule yao kutoana na makazi ya wazazi wao kuchomwa moto na Wasonjo. Watoto hao wamepelekwa kufanya mtihani katika Shule ya Sekondari Loliondo.
Gazeti lako linafunga macho na masikio; lakini kweli itashinda!
-- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 Comments