Mshauri wa biashara Charles Nazi na mtunzi wa kitabu cha mbinu za biashara na maarifa ya kupata pesa na utajiri, ameanzisha program ya miezi 18 ya kuwasaidia watu wenye malengo ya kutafuta utajiri kufanikisha malengo yao kwa gharama nafuu. Mfumo kama huu umesaidia watu wengi duniani hasa katika nchi zilizoendelea kwa haraka sana. Kwa mfano Anthony Robins huko Marekani alibadilisha maisha yake kutoka kwenye umasikini alivyokuwa akiishi kwenye nyumba ya kupanga na kuwa milionea kwa muda wa miaka 3. Aliweza kufanikiwa namna hii baada ya kumpata mwalimu Mentor aitwaye Jim Rohn. Ukitaka habari zaidi za watu hawa wawili unaweza kuzipata kwenye Google.
Kuna njia mbili za kutafuta utajiri njia ya kwanza ni ya kuhangaika mwenyewe bila msaada wowote hii ni njia ndefu. Njia ya pili ambayo ni fupi ni kutafuta Mwalimu,mshauri wa biashara mwenye mafanikio wa kukuongoza. Kwa kiingereza anaitwa (Mentor)
Namna ya kupata mshauri na Mwalimu (Mentor) wa biashara katika Tanzania
Kama unatafuta huduma ya mshauri/mwalimu (Mentor) ni muhimu kutafuta yule mwenye uzoefu na sifa nzuri. Kuna njia mbalimbali za kupata mshauri wa biashara. Katika ngazi ya msingi sana, unaweza kumpata kutokana na ushauri wa mfanyabiashara ambaye amewahi kupata huduma kutoka kwa mshauri fulani kwa mafanikio. Unaweza kupata ushauri kutoka kwa mfanyabiashara maarufu ambaye atakuwa tayali kutumia muda wake.(Kitu ambacho ni kigumu)
Kama wewe unashindwa kulipia huduma za ushauri hicho siyo kikwazo, kuna idadi ya mashirika na makampuni binafsi ambayo hutoa ushauri bure au kwa bei nafuu. Ukweli ni kwamba kwa kuwa huduma zao ni bure au za bei nafuu haina maana wao hawana sifa au uzoefu. Baadhi ya wataalamu na washauri wametoa ushauri kutoka huko nyuma kwa jamii zao na kupata uzoefu kama mkufunzi au mshauri, Charles Nazi ni mshauri wa biashara mwenye sifa hizo.
Programu ya Utajiri.
Utangulizi
Programu ya utajiri ni mpango wa kutoa ushauri na msaada kwa watu wote wenye malengo ya kutafuta utajiri kwa njia halali. Wajasiriamali hufanyiwa tathmini, kuangalia shughuli wazofanya au biashara wanazotaka kuanzisha kisha kuendelea kupata ushauri kwa kipindi cha miezi 18 ili kusaidia ukuaji wa biashara zao na kuzifanya ziwe endelevu.
Malengo ya mpango.
• Kuhamisha ujuzi wa biashara na maarifa miongoni mwa wajasiriamali wa Tanzania
• Kuongeza fursa endelevu na ukuaji wa biashara
• Kutoa jukwaa kwa ajili ya uchumi mdogo kuchangia katika uwezeshaji wa uchumi mkubwa.
Kwa nini kuwe na mpango huu?
Duniani kote biashara nyingi huanza kwa msaada wa kifedha wa familia na marafiki,pamoja na msaada huu kwa kawaida huja na ushauri wa biashara pia ushauri wa upatikanaji wa masoko. Mpango huu ni programu ya kujaza nafasi ya familia kwa ajili ya watu wasio na ajira na kujiajiri hasa vijana kina mama na watu wote wasio na uwezo.
Lazima tutambue kwamba changamoto ya kuanzisha biashara, kupata vyanzo vya mitaji mara nyingi ni kazi ngumu, na muda mwingi hutumika kwa ajili ya kutafuta mbinu za kuanzisha biashara. Mara biashara inapoanza changamoto nyingine huzuka nazo ni kuifanya biashara iweze kuanza kupata faida kwa kutafuta masoko ili uweze kuuza sana na kulipia gharama zikiwepo za uendeshaji na hata kulipia mikopo ambayo ina riba kubwa. Kwa changamoto hizi mjasiriamali mdogo hana uwezo wa kulipia gharama za mshauri wa biashara ambaye anatoza gharama kubwa. Mpango huu unawasaidia wajasiriamali wadogo kupata ushauri mzuri wa kuwasaidia kuanzisha na kuendesha biashara zao kwa ufanisi.
Uzoefu na uwezo wa Mshauri charles Nazi
Charles Nazi ni msomi mwenye stashada ya Uhasibu kutoka kwenye bodi ya Wahasibu na wakaguzi. Ana uzoefu wa miaka 24 katika kazi ya ukaguzi. Amekuwa kiongozi wa SACCOS kwa miaka 20. Pia ni mjasiriamali ambaye amefanya shughuli mbali mbali na kubuni miradi mbali mbali, kwa mfano amewahi kuanzisha kwa ubia kampuni ya Ujenzi iliyojulikana kwa jina la, Shinyanga annex Building contractors, kiwanda kidogo cha chaki, kuendesha biashara ya mtandao kupitia Makampuni mbali mbali ya kigeni, biashara hizi ameachana nazo. Sasa hivi anajishughulisha na kutoa huduma ya Ushauri wa biashara. Huduma ambazo anazitoa ni; Kutoa ushauri wa biashara kwa Wafanyabiashara wadogo wa kati na wakubwa, Kuandaa michanganuuo kwa ajili ya kuomba mikopo benki na misaada kutoka kwa wafadhili, Kutoa mafunzo ya Ujasiriamali kwa wafanyabiashara, Kuandaa mifumo ya utunzaji wa mahesabu na kuweka mifumo ya Kompyuta kwenye utunzaji wa hesabu, Kuandaa katiba za vyama na nyaraka za uandikishaji wa makampuni, Kuandaa nyaraka za Tenda, Kutoa ushauri kwa SACCOS ili ziendeshwe kwa ufanisi, Kutoa ushauri kwa Asasi zisizo za kiserikali NGO ili ziweze kuendesha shughuli zao kwa ufanisi, Kutoa ushauri nasaha na semina kwa wanafunzi.
Charles Nazi ni mtunzi wa vitabu na ametunga kitabu cha Ujasiriamali kinachopendwa sana, kiitwacho, Mbinu za biashara na maarifa ya kupata pesa na utajiri. Kitabu hicho kinalenga kumsaidia mtu yeyote ambaye anatafuta utajiri kwa kufanya biashara ndogondogo hadi kubwa. Pia kinatoa maarifa, mbinu na mikakati mbalimbali ya kupambana na umaskini, kinatoa elimu ya biashara na mbinu mbalimbali za namna ya kupata pesa kwa njia halali ili kukurahisishia safari yako ya kuelekea kwenye kutafuta na kupata utajiri. Kitabu hicho kilichapishwa kwa mara ya kwanza na Business Printers mwezi March mwaka 2008 na mpaka sasa zimechapishwa na kuuzwa nakala 4,000. Amewawezesha wajasiriamali kupata mikopo ya shilingi milioni 400 kutoka katika mabenki kwa kuwaandikia michanganuo ya biashara. Amewasaidia watu wengi kuweza kuinuka kupitia kitabu chake, semina, ushauri, simu na vipindi vya redio na televisheni.
Hitimisho
Programu hii inapatikana kwa ghrama ya sh. 300,000.00 kwa kipindi chote cha miezi 18. Kwa kujiunga na program hii utapata huduma zifuatazo;
Kitabu cha mbinu za biashara na maarifa ya kupata pesa na utajiri.
Tathmini ya wazo la biashara au biashara yako ili kuweza kujua uanze vipi na kujua vikwazo vinavyokukwamisha usianze au kusogea mbele.
Mafunzo ya ujasiriamali ambapo utapata fursa ya kuuliza maswali na kupata majibu papo hapo.
Ushauri kwa kipindi chote cha mkataba
Mawasiliano ya karibu na mshauri kwa simu au email unapopatwa na vikwazo katika biashara yako.
Mbinu za hali ya juu za uwekezaji ili kupanua uwezo na kuongeza mtaji wako.
Kuunganishwa kwenye mtandao wa wajasiriamali wateja wake ili kubadilshana mawazo.
Je, wewe unataka kuwa tajiri?
Tafadhali wasiliana CHARLES Nazi mshauri Biashara Dar es salaam kwa maelezo zaidi tafadhali piga 0755394701 pia tembelea blog yake katika; http://www.squidoo.com/mshauricharles
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
1 Comments
Are you suffering financially or do you need an urgent cash to pay your bills? And you want to take the risk of transforming your own life. Try and get your ATM blank card today and be among the lucky one's who are benefiting from this card. This ATM card is set capable of hacking into any ATM machines anywhere in the world. I have to know about this blank ATM card when I was looking for work online about a month ago. It has really changed my life forever and now I can say I'm rich because I am a living testimony. The less money I get in a day with this card is $3,000. Even now and then keep pumping money into my account. Although the card is illegal but there is no risk of being caught. It is programmed in such a way that it cannot be tracked and also has a technique that makes it impossible for the CCTV camera to detect you when using it. For details on how to get yours today contact speedhackersnetwork001@gmail.com
REPLY