Uchunguzi nilioufanya kwa muda wa mwezi mmoja sasa nimepata taarifa za
uhakika kuwa dawa za kulevya zinaingizwa Tanzania Bara Kupitia Kisiwa
cha Unguja, Katika Uchunguzi huo nimebaini kuwa wanawake ndiyo
wabebaji wakubwa wa dawa hizo kutoka Unguja na Kufikisha Dar es
salaam, Wanatumia umakini sana katika ubebaji wa madawa hayo hatari
wanaficha kwenye nguo zao za ndani na juu wanavaa baibui na mitandi
kichwani ili wasigundulike na ofisa usalama Bandarini.
Taarifa zaidi nimeambiwa na rafiki yangu…………………………………………..ambaye ni
mfanyabiashara wa mchele kutoka Kahama na kupeleka Unguja, ameniambia
kuwa Bandari ya Zanzibari maafisa wa jeshi la polisi mara nyingi
hawafanyi upekuzi wa watu wanaotoka unguja kuja Dar es salaam kwa
usafiri wa Boti, amezidi kunifahamisha kuwa hivi sasa Zanzibari ndiyo
njia kuu ya kupitisha madawa hayo hatari ni baada ya vyombo vya
usalama Tanzania bara kudhibiti kwenye viwanja vya ndege na maeneo
mengine ya mipakani.
Soko la mauzo la madawa hayo hatari ni Magomeni mwembe chai Katika
uchunguzi niliofanya nimegundua siko la madawa ya kulevya eneo la
mwembe chai , eneo hilo ambalo nimechora ramani inayoonyesha nyumba
inayotumika kuwauzia wateja wao ambao ni watumiaji wa madawa hayo
hatari ambayo wateja wao wakuu ni vijana,kwenye nyumba hiyo ambayo ni
jumba la kienyeji kuu kuu ndani wapo wanawake ambao ndio wauzaji
wakubwa pamoja na wanaume wachache.
Nashauri ufanyike uchunguzi na kudhibiti uingiaji wa madawa hayo
kutoka zanzibari kupitia Bandari ya Zanzibari, na Uchunguzi mwingine
ufanyike katika eneo la mwembe chai kwenye soko la wateja wanaotumia
madawa hayo hatari
RIPOTI 2
Tarehe 20/06/2012 saa saba mchana ndugu ……………………………………………ambaye yupo
mahabusu ya keko aliwasiliana na mwenye simu namba 0715 137070 ambaye
yupo uraiani, uchunguzi nilioufanya nimefanikiwa kupata namba ya simu
inayomilikiwa na mtuhumiwa aliyepo mahabusu ni namba 0652486272
imesajiliwa kwa jina la Ally Njegite, wakati
mtuhumiwa……………………………………………………….Akiwasiliana na mpenzi wake (Bibi)
kutaka kujua taratibu za kumdhamini wakati atakapo letwa mahakamani
zimefikia wapi.
Uchunguzi nilioufanya kuanzia Geraza la Keko na Baadhi ya watu ambao
waliwahi kushikiriwa mahabusu ya Keko wamaniambia kuwa mahabusu na
wafungwa wanaotumia simu wakiwa ndani simu hizo zinaingizwa na Askari
magereza ,zikitokea kwa ndugu wa mahabusu hao walioko uraiani.
Mahabusu uwatuma askari magereza kwenda kwa ndugu zao
kuwachukulia pesa na kupewa simu hatimaye huwaletea mahabusu na
kuwakabidhi.
Aidha wameniambia kuwa kwenye selo au vyumba vya mahabusu
hakuna soket ya kuchaji simu kutokana na usalama wa mahabusu
na wanafungwa, simu hizo uchajiwa na askari magereza.
Nashauri uchunguzi ufanyike kugundua simu zilizoko gereza la
keko moja ya simu hiyo no. 0652 486272 na mtandao baadhi
ya askari magereza ambao sio waaminifu wanaoingiza simu kwa
mahabusu na wafungwa wajulikane na hatua za kinidhamu
zichukuliwe kwani wanahatarisha usalama wa magereza .
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 Comments