[wanabidii] NENO WAHANGA

Friday, August 24, 2012
Ndugu wachangiaji mada humu ndani,
Naomba tena tusaidiane kuweka neno "Wahanga" litumike kama inavyotakiwa. Mara nyingi waandishi wa habari na watangazaji na sisi pia tunalitumia vibaya.
 Wahanga limetokana na neno Mhanga na maana yake ni mtu au kikundi cha watu kujitolea hasa kufa au kufanya maafa fulani.
Sasa sisi tunaposema wahanga wa ajali  au wahanga wa mafuriko tunakosea kwani hao wanaopata ajali hawakujitolea ila imewakuta.
kwahiyo sio vizuri kusema wahanga wa ajali bali waathirika wa ajali. Mwenye mawazo tofauti anaweza kutuelimsha zaidi

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments