[wanabidii] Kwa nini Polisi wana uhuru wa kufanya lolote bila kuchukuliwa hatua?

Tuesday, August 28, 2012
Nimekuwa najiuliza kwa nini Polisi hata wakiua kwa makusudi hawachukuliwi hatua? Mawaziri na Makatibu Wakuu wanaondollewa katika nafasi zao wakiwa na tuhuma, wakurugenzi wa Idara za Serikali na mashirika ya umma wanasimamishwa kazi kukiwa na tuhuma kuwa wamekiuka miiko ya kazi zao.
 
Cha ajabu Polisi wanavyopendwa na mkuu wao wakiwa na tuhuma za kushirikiana na majambazi wanahamishwa na kupandishwa vyeo. Polisi hao hao jana huko Morogoro wamemuua muuza magazeti kwa kumpiga risasi kisogoni. Hii ni "Cold Blooded Murder".
 
Naomba wanabidii wenzangu mniambie kwanini Polisi wanapendelewa hivi? 

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments