Dar es Salaam, Jumanne, Machi 3, 2015 – Serikali ya Tanzania itatoa taarifa ya Utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa! (BRN), Alhamisi; tarehe 5 Machi 2015, kuhusu utekelezaji wa mikakati iliyowekwa katika Sekta Sita za Kipaumbele (NKRAs) zilizotekelezwa katika mwaka 2013/14. Sekta hizo ni: Kilimo, Elimu, Nishati, Uchukuzi, Maji, na Utafutaji Raslimali Fedha.
Ripoti ya Mwaka ya BRN imeandaliwa kuendana na utamaduni wa BRN wa kuweka vipaumbele, malengo na mfumo wa utekelezaji unaoendana na uwekaji wa mikakati ya kina ya kusimamia ufuatiliaji; pamoja na utumishi makini wa wafanyakazi wanaosimamia na kutekeleza kwa uwazi.
Umma unaalikwa katika maonesho ya miradi ya BRN yatakayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City kuanzia saa saba mchna hadi saa 11 jioni ili kupata fursa ya kuufahamu zaidi mfumo huu na mikakati inayoendelea kutekelezwa.
Katika tukio hilo wananchi pia watapata fursa ya kukutana na watekelezaji pamoja na walengwa wa miradi ya BRN, ambao watazungumzia uzoefu wao kuhusu safari ya mabadiliko wanayoiona na jinsi mabadiliko ya kiutendaji yaliyoletwa na BRN yanavyoboresha maisha yao.
Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huu.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments