Ndugu zangu,
Nimekuwa najiuliza kwa nini CCM wanauchukia mfumo wa Serikali tatu kiasi cha kufikia kuupinga "ruthlessly, violently na abusively"!
- Mmesikia viongozi wa CCM wakiwa "encourage" wanajeshi kuchukua nchi kama mfumo wa Serikali tatu utapita!
- Mmewasikia viongozi wa CCM wakiwaamrisha Green Guard kuwapiga UKAWA!
- Mmewasikia viongozi wa CCM wakitishia kuingia msituni kama mfumo wa Serikali tatu utapita!
- Mmewasikia viongozi wa CCM wakiwaita UKAWA watoto wa shetani!
- Mmewasikia viongozi wa CCM wakiwaita UKAWA Boko Haram!
- Mmesikia kiongozi mkubwa kabisa wa CCM akitamka kuwa chama chake hakihitaji katiba mpya!
Hebu tuambieni mlio karibu na CCM mfumo huu wa Serikali Tatu una matatizo gani kiasi ambacho wenye nchi wanauchukia kuliko wanavyowachukia MAJANGILI na WAUZA UNGA.
Nawasilisha.
0 Comments