[wanabidii] Pengo aonya wahuni pasaka

Thursday, March 28, 2013

Na Tanpress

ASKOFU Mkuu wa jimbo kuu katiliki Dar es Salaam, mwadhama,Kardnali Pengo,amesema kuwa haamini kama vurugu za kidini zinazotokea hapa nchini zinasababishwa na mgawanyiko wa kidini.
Akitoa salamu  za pasaka kwa wandishi wa habari askofu Pengo ameweka wazi kuwa kinachotofanyika sasa ni kikundi cha  wahuni wachache ambao wamejitwalia madaraka kama vile serikali haipo.
"HATUWEZI kukubali nchi itawaliwe na kikundi cha wahuni waliojitwalia madaraka ,kama vile nchi haina serikali na kuwaacha wahuni watawale"alisema Pengo
Ametoa wito kwa pande tatu za wakiristo, waislam na serikali kukutana haraka kujadiliana namna ya kukomesha hali hiyo ili amani iendelee kuwepo badala ya wananchi kuishi kwa hofu.
"tukitaka kujadiliana kila upande uwe tayari kupokea maoni ya upande mwingine kwa nia njema ndio tutamaliza tatizo hilo"
Hata hivyo amesekitishwa na kitendo cha serikali kushindwa kumkamata mtu au w atu waliohusika kumwangamiza Padri mushi aliyepigwa risasi Febrari 17 Mwaka huu mjini Zanzibar.
'hali hii ikiachwa iendelee hivyo hivyo bila kvyombo vya usalama kutoa ripoti walipofikia uchunguzi wao inaweza kuleta matatizo.  

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments