[wanabidii] TAARIFA YA UBALOZI WA TANZANIA CHINA KUHUSU JACKIE CLIFF KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA

Friday, January 10, 2014
Mwezi December 2013 taarifa zilitoka kwamba kuna binti wa Kitanzania mwenye umri wa miaka 28 aliekamatwa na dawa za kulevya huko Macao China ambapo baadhi ya taarifa zilizoripotiwa na Waandishi wa Tanzania zilisema aliekamatwa ni mrembo ambae amekua akionekana kwenye video kadhaa za wasanii wa bongofleva (Jackie Cliff).
Ubalozi wa Tanzania nchini China umezungumza na kusema yafuatayo ...

'Uongozi wa hapa haujatujulisha chochote wala kutuandikia, kwa taratibu zetu sisi kama balozi watu wote ambao wanakamatwa hapa kwa makosa ya aina yoyote ile serikali husika zinatuandikia, zikituandikia zinasema alikamatwaje na walichukua/watachukua hatua zipi, na kama wameshamfungulia mashitaka wanatujulisha, mpaka sasa hatuna taarifa yoyote kutoka kwa Serikali kuhusu hilo la Jackie

Mara ya mwisho kupata taarifa za Mtanzania kukamatwa na dawa za kulevya China ilikua lini?

Balozi: 'Ninazo taarifa nyingi ila ni kama mwezi uliopita alikamatwa Mwanaume, ni Wanaume waliokamatiwa Guangzhou, mtu wangu aliekua anafatilia pia amekuja leo January 9 2014 asubuhi na kuniambia hakuna taarifa zozote kuhusu Jackline Patrick Cliff'

Kama ni Macao wangetuandikia moja kwa moja, Macao na Hongkong wangetuandikia moja kwa moja na kama wangekua wamewasiliana na balozi wetu wa heshima kule Hongkong pia wangetuandikia, Wachina mtu yeyote wanaemkamata ambae anatumia hati ya kusafiria ya Tanzania wanamuhusisha kama raia wa Tanzania kwa hiyo wanajulisha ubalozi wake labda mtu mwenyewe aseme ni wa taifa jingine, watatuandikia hivyohivyo nakueleza…

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments