[wanabidii] POLISI UJERUMANI WAMUOKOA DIAMOND KUTOKA KWA WASHABIKI WENYE HASIRA !

Sunday, August 31, 2014 Add Comment





UJERUMANI SI SHWARI KIMENUKA !!

POLISI UJERUMANI WAMUOKOA DIAMOND KUTOKA KWA WASHABIKI WENYE HASIRA ! KASHINDWA KUWIKA STUTTGART KISA NA MKASA ?!

KAFIKA UKUMBINI SAA 10 ALFAJIRI ! WASHABIKI WANASURI SHOW TANGU SAA 4 USIKU

PROMOTA MNAIJERIA AINGIA MITINI ,DJ APATA KISAGO HETI VYOMBO VIBOVU ! HAIBU

Stuttgart,Ujerumani,
Usiku wa Jumamosi ya Tarehe  30.Augost 2014, majira ya saa 10 alfajiri
Mwanamuziki nyota wa Bongo Flaver  Nasib Abdul aka Diamond Platnumz alijukuta katika hali ya hatari hadi kuokolewa na Polisi mjini Stuttgart,ujerumani,baada ya washabiki waliokuwa na hasira kuchoka kusubiri show,washabiki hao waliokuwa wamelipa ticket euro 25 kwa kiingilio walihadiwa kuwa show ingeanza saa 4.00 usiku,lakini walijukuta wakisubiri hadi majira ya saa10 usiku au alfajiri ndipo mwanamuziki Diamond alipoletwa jukwaani na promota wake raia wa Nigeria anajiita kama Britts Event.
Hapo ndipo washabiki walipoona kuwa hawakutendewa haki walianza kurusha chupa na kutaka kumvamia mwanamuziki  Diamond na promota wake,
Kilichowakera zaidi washabiki ni pamoja na vyombo vibovu vilivyofungwa katika ukumbi huo kitu ambacho kiliwafanya washabiki kuvunja hadi vyombo vya muziki
ma-Djs walishambuliwa na wapo Hosptalini kwa sasa.moja wa Djs hao alipoteza Lap top yake ,mwanadada DJ  Flor alipatwa shock mstuko wa moyo na kukimbizwa hosptali, washabiki hao walimpa kipigo  DJ Drazee naye yupo hoi hospatal. Polisi nchini ujerumani wanamesema tukio hili la haibu alijawahi kutokea,kuwa msanii kuchelewa kufika jukwaani kwa ujerumani ni kitu cha hatari kwani washabiki wa ujerumani wanaheshimu sana muda wao.
mpaka sasa polisi wanamsaka mwandaaji wa onyesho hilo na wamesema kuwa
wanachunguza thamani ya hasara hiliyosababishwa na ghasia hizo na pia itamfungulia mashataka promoter huyo raia wa Nigeria,ambaye pia anachunguzwa kwa kusemekana anajihusisha na mtandao fulani wa biashara.

Magazeti ya Stuttgart; yameandika "Washabiki wa hasira nawe DIAMOND"  link:



--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

[Mabadiliko] CCM SASA WASIKIE

Sunday, August 31, 2014 Add Comment
[Mabadiliko] CCM SASA WASIKIE
Jukwaa la Waktisto Tanzania limetoa waraka mzito kwa Rais na viongozi wa CCM, kuhusians na kile kinachoendelea ktk bunge maalumu la katiba. Ktk waraka huo, wamesema kinachofanyika sasa bungeni ni usaliti mkubwa, kutojali maslahi ya nchi na kinahatarisha amani ya nchi. Wamemtaka rais kusitisha mara moja vikao na "rais aiokoe ccm na kuwafanys watanzania wasikichukie chama hicho. Shida, watasikia ushauri
Sent from my Huawei Mobile

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com


For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/oq4b03b9wif7utna3msk9uin.1409495974953%40email.android.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

[wanabidii] Burn your ISIS flag, French shul bombing foiled, Syrian drone shot down - Aug. 31, 2014

Sunday, August 31, 2014 Add Comment
[wanabidii] Burn your ISIS flag, French shul bombing foiled, Syrian drone shot down - Aug. 31, 2014

Email look weird? View it on the web here .

August 31, 2014 / 5 Elul 5774

Cartoons


Click Here!

Headlines & Recommended

IDF Shoots Down Syrian Drone with Patriot
The IAF shot down a drone from Syria...
A Patriot Missile System in Israel


Teen Girls Planned to Bomb French Synagogue
The jihad network has snared teenagers in its web. One out of every six Frenchmen supports the ISIS.
The Great Synagogue in Lyons was targeted for a suicide bombing by two Muslim teenage girls.


Burn Your ISIS Flag Today [video] #BurnISISFlagChallenge
Burning ISIS flags is starting to go viral in Lebanon, but the Lebanese Justice Minister wants to make it illegal.
#BurnISISFlagChallenge


Zoabi Sings Palestinian Authority Anthem at Hamas 'Victory' Rally
What other country would allow legislators to openly declare their allegiance to another entity?
MK Hanin Zoabi, under the protection of the Israeli flag, speaks against Israel.


Tensions with Catholics Force Lev Tahor Out of Guatemala Village
Mixing the Haredi Lev Tahor cult with a bunch of fiercely religious Roman Catholics is a recipe for dynamite.
Lev Tahor children, in black garb, play with their toys.


British Jews To March Against Anti-Semitism
With Judeophobic attacks spiking around United Kingdom, local Jews say not enough done to enforce hate crime laws
Man holds daughter on shoulders at Pro-Israel Rally


Read more Headlines & Recommended articles
 



Click for your Print subscription to The Jewish Press .


Forward this email to a friend .

Received this from a friend? Subscribe .

We hope you won't, but if you must, you can unsubscribe instantly from these emails by clicking here.

[wanabidii] Usahihishaji mpya sekondari waanza

Sunday, August 31, 2014 Add Comment
[wanabidii] Usahihishaji mpya sekondari waanza
*Ukadiriaji wanafunzi wakifeli wazikwa rasmi
*Mfumo upangaji madaraja nao wabadilishwa  
*Utaanza na mtihani wa 'moko'  kidato cha nne

USAHIHISHAJI mpya wa mitihani ya Taifa kwa kidato cha nne na sita, unaoendana na utaratibu mpya wa upangaji wa ufaulu na madaraja, unatarajiwa kuanza kutumika katika mtihani wa majaribio wa kidato cha nne mwaka huu nchini kote, na kufuatiwa na mitihani yote ya kidato cha nne na sita.
Akitangaza mabadiliko hayo muhimu jana Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani (Necta), Dk Charles Msonde, alisema tayari maelekezo kuhusu mabadiliko hayo, yameshatolewa kwa wakuu wa shule za sekondari nchini.
Baadhi ya faida ya mabadiliko hayo kwa mujibu wa Dk Msonde, ni pamoja na kuondoa ukadiriaji wa alama za ufaulu, uliokuwa ukitumiwa awali, kuweka uwazi katika usahihishaji na kumwezesha mwanafunzi kukokotoa ufaulu wake hata kabla ya matokeo na hata mwalimu kukotoa ufaulu wa wanafunzi wake kabla hata ya matokeo.

Kwa mujibu wa Dk Msonde, mwalimu na mwanafunzi wataweza kukokotoa alama za ufaulu, kwa kuwa majibu yanayotumika kusahisha mitihani kila mwaka na namna wanafunzi walivyojibu, yatarejeshwa shuleni, ili mwalimu afahamu hali ya wanafunzi na ufundishaji.

Pili kwa mujibu wa Dk Msonde mabadiliko ya sasa, yatamwezesha mwalimu kufahamu shida ya wanafunzi wake kulingana na taarifa ya ufaulu wa waliopita na kufahamu wapi patumike mbinu gani kuinua ufaulu.


  *Ukadiriaji 
Kwa mujibu wa Dk Msonde, mabadiliko hayo yanaanza katika mfumo wa viwango vya ufaulu, kutoka katika Mfumo wa Viwango vya Ufaulu Vinavyobadilika, kwenda katika Mfumo wa Viwango vya Ufaulu Visivyobadilika.
Mfumo wa Viwango vya Ufaulu Vinavyobadilika, Dk Msonde alisema ulianza kutumia tangu mwaka 1973, wakati Necta ilipoanzishwa mpaka 2011.
Akifafanua kuhusu mfumo huo ulioachwa mwaka 2011 na kuzikwa rasmi kuanzia mwaka huu, Dk Msonde alisema wanafunzi wakifeli sana, Necta ililazimika kukadiria viwango vya ufaulu kuwa vya chini kabla ya kutoa matokeo.
Alisema walikuwa wakiangalia wastani wa ufaulu na kulinganisha na mwaka uliopita, kama ni wa chini  waliangalia waliofaulu sana na waliofeli sana, kisha waliangalia tofauti ya alama ya ufaulu kati ya waliofaulu na baada ya hapo walikuwa wakibadilisha viwango vya ufaulu kuwa vya chini kabla ya kutoa matokeo.
Alitoa mfano, kama mwaka uliopita wastani viwango vya ufaulu wa somo kama Historia ulikuwa 60 na mwaka huo wastani huo ukashuka kuwa 40, ilikuwa ishara ya kwanza kuwa somo husika mwaka huo wamefeli sana.
Kutokana na hali hiyo, alisema kama alama A ilianzia 80 mpaka 100, Necta iliweza kushusha ianzie 70 mpaka 100, ili hata waliopaswa kuwa na alama B, wapande kidogo na hivyo hivyo katika alama zinazofuata.
"Hivyo katika mfumo huu, viwango vya ufaulu hupangwa kwa kutegemea watahiniwa walivyofaulu somo husika, hivyo viwango hivyo vya ufaulu hutofautiana baina ya somo na somo na kati ya mwaka mmoja na mwingine," alisema Dk Msonde.
Matokeo yake, Dk Msonde alisema viwango vya ufaulu vilikuwa siri na Baraza halikuwahi kueleza popote kuhusu usiri huo na wadau walikuwa na habari za kupotosha kuwa A ilikuwa inaanzia 81 na D ikianzia 21, wakati katika hali halisi kuna wakati viwango hivyo vilishuka.
*Kuzika ukadiriaji
Kuanzia mwaka huu Mfumo wa Viwango vya Ufaulu Visivyobadilika, unaanza kutumika na viwango hivyo ni vipya baada ya kupangwa kwa kuangalia mwenendo wa ufaulu wa miaka 12, kuanzia 1999 hadi 2011.
Dk Msonde alisema katika miaka hiyo 12 ya kuangalia, A ya juu ilikuwa mwaka  1999 na 2011, ambapo ilianzia 70 mpaka 90. Alisema hakuna mwaka A ilishuka chini ya 70. Alama D katika miaka hiyo 12, ilianzia 30 mpaka 45.
Baada ya kupata alama hizo, Dk Msonde alisema walitafuta wastani wa A katika miaka hiyo 12 ambao ulikuwa ni 76.2 na wengi waliopata A ya chini katika muda huo ilikuwa 75.
Katika kutafuta wastani wa D katika miaka hiyo 12, ulikuwa 33.3 na D iliyotumika sana katika miaka hiyo ilikuwa 30 ndipo wakaamua kuweka viwango vipya vya ufaulu.

*Viwango vipya
Baada ya wastani huo, Dk Msonde alisema walianza kupanga viwango vipya vya ufaulu ambavyo vitatumika katika usahihishaji wa mtihani wa taifa wa kidato cha nne na mtihani wa taifa wa kidato cha sita, ambao hautakuwa na tofauti katika ya mitihani hiyo.
Kabla ya viwango hivyo, kidato cha sita kilikuwa na alama saba za ufaulu, yaani A, B, C, D, E, S na F wakati kidato cha nne kilikuwa na alama sita za ufaulu, yaani A, B, C, D na F.
Katika viwango vipya kutakuwa na alama saba za ufaulu kwa mitihani yote ya kidato cha nne na kidato cha sita, ambayo ni A ambayo itaanzia (75-100), tafsiria yake ni Bora sana.
Kutakuwa na B+ (60-74, vizuri sana); B (50-59, vizuri); C (40-49, wastani); D (30-39, inaridhisha); E (20-29; hairidhishi) na F (0-19, amefeli).
* Madaraja zamani
Mbali na mabadiliko katika viwango vya ufaulu, mabadiliko mengine yaliyofanyika ni katika ukokotoaji wa madaraja ya ufaulu, kutoka Mfumo wa Ukokotoaji wa Jumla wa Pointi (TPGS), ambao umekuwa ukitumiwa tangu 1973 mpaka  2014 kwenda Mfumo wa Wastani wa Ukokotoaji wa Pointi (GPA) utakaotumika katika matokeo ya kidato cha nne ya mwakani.
Katika mfumo wa TPGS, alama A ilikuwa na pointi 1; alama B+, pointi 2; B, pointi 3; C pointi 4; D pointi 5; E pointi 6 na F pointi 7.
Kwa kuwa upangaji wa madaraja, uliangalia masomo saba ambayo mwanafunzi alifaulu zaidi, mwanafunzi aliyefaulu sana katika mfumo huo, kwa maana ya kupata alama A masomo yote saba, alipata Daraja la Kwanza lenye pointi  saba, kwa maana na kila somo  pointi moja.
*Madaraja mapya
Katika mfumo wa GPA, Dk Msonde alisema alama A inakuwa na pointi 5; B+, pointi 4, B pointi 3; C pointi 2; D pointi 1; E pointi 0.5 na F pointi 0. Katika hilo, mtahiniwa ataanza kuhesabika amefaulu somo endapo atapata alama D, ambayo ni sawa na pointi 1.
Akielezea namna alama hizo zitakavyotumika kupanga madaraja, Dk Msonde alisema mfumo utakuwa kujumlisha alama za ufaulu za mwanzo katika masomo saba na kugawanya kwa saba, hivyo mwanafunzi atakayefaulu sana na kupata alama A katika masomo saba, atapata jumla ya alama 35, ambayo ikigawanywa kwa masomo hayo saba, atapata pointi 5, ambayo ndiyo utaulu wa juu utakaoitwa 'Distinction'.

Hivyo madaraja mapya kwa kidato cha nne yatakuwa daraja la kwanza 'Distinction'  pointi (3.6-5.0);  pili 'Merit' (2.6-3.5); tatu 'credit' (1.6-2.5); nne pass (0.3-1.5) na aliyefeli 'fail' (0.0-0.2).

Kwa kidato cha sita, atakayefaulu sana kupata A katika masomo matatu ya 'combination', atakuwa amepata jumla ya pointi 15 na ukigawanya kwa tatu, yaani masomo matatu ya 'combination', naye atapata 5.

Hivyo madaraja mapya kwa kidato cha sita yatakuwa daraja la kwanza 'Distinction' pointi (3.7-5.0); pili 'Merit' (3.0-3.6); tatu 'Credit' (1.7-2.9); nne 'pass' (0.7-1.6) na aliyefeli 'fail' (0.0-0.6).
 source:Habarileo

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

[wanabidii] CYBER BULLYING - UNYANYASAJI KWENYE MITANDAO

Sunday, August 31, 2014 Add Comment
[wanabidii] CYBER BULLYING - UNYANYASAJI KWENYE MITANDAO

CYBER BULLYING – UNYANYASAJI KWENYE MITANDAO 


Betty Ndejembi ni msichana mrembo na mwanamitindo , anatumia sana huduma za mitandao ya kijamii kwa ajili ya shuguli zake mbalimbali za kujiingizia kipato na kujitangaza zaidi .


Siku moja alibakwa mpaka akapoteza fahamu , akaokotwa na watu akapelekwa hospitali , alipofika hospitali aliendelea kutumia mitandao ya kijamii kwa ajili ya kufahamisha wenzake anavyoendelea kwa nia nzuri kabisa .


Jinsi alivyokuwa anafahamisha umma kuhusu maendeleo yake ndio baadhi yao walitumia fursa hiyo kumtukana , kumnyanyapaa , kutumiana picha zake na dhihaka nyingine nyingi kwa njia ya mitandao hiyo hiyo .


Msichana Betty alifariki dunia baadaye wakati anaendelea na matibabu , lakini matusi aliyovurumishiwa , maneno aliyoambiwa na unyanyasaji mwingine umeleta historia mpya katika matumizi salama ya mitandao ya mawasiliano .


Jijini arusha  kijana mmoja kutwa na mke wa mtu , akadhalilishwa huku akipigwa picha , zile picha zikawekwa kwenye mitandao kadhaa ya kijamii , baada ya siku chache yule kijana alionekana amejinyonga chini ya daraja .


Huko marekani dada mmoja anayeitwa Rebecca Ann Sedwick , aliamua kujitoa uhai baada ya kudhalilishwa kupitia mtandao wa kijamii unaoitwa Ask FM na Kik Messenger .

 

Kitendo alichofanyiwa Betty na huyo Kijana kwa kiingereza kinatwaita CyberBulling yaani mtu kutumia njia za mawasiliano kwa nia ya kuumiza , kudanganya au kumdhalilisha mwingine , labda kwa maneno , picha , sauti , video na vingine vingi .


Vitendo hivi ni kama kutumia picha ambayo mwenye nayo hajaruhusu , kuandika habari za uwongo haswa za udaku , kuuandika au kutoa maoni ambayo si ya kweli kwa nia ya kudhalilisha au kuumiza , kudanganya kuhusu bidhaa au huduma Fulani kwa nia hiyo hiyo .


Tafiti mbalimbali zilizofanyika zinaonyesha watu wengi wanaohusika katika matukio ya unyanyasaji kwa njia za mitandao ni vijana au makundi ya vijana pia zimeeleta madhara haswa vifo .


Mimi binafsi niliwahi kukumbana na sakata kama hili , lakini ilimkuta rafiki wa rafiki yangu mmoja , yeye alikuwa na mpenzi wake , kumbe wakiwa kwenye starehe yule mwanaume alikuwa na tabia za kumpiga picha .


Siku ikafika hawakuelewana ikabidi kila mtu aendelee na maisha yake , yule kijana akaingia facebook akatengeneza jina bandia akaweka picha za yule binti na kuwarushia watu wa karibu wa binti halafu akafuta lile jina .

Binti alienda polisi kutoa taarifa , polisi wakaomba ushahidi wa picha , lakini ndio hivyo jamaa alikuwa ameshafuta mpaka jina , kwahiyo wakaomba msaada , nikawapeleka polisi makao makuu kitengo cha CYBERCRIME .


Polisi waliweza kupata taarifa zote zinazohusu yule kijana kwenye mitandao ya kijamii na wakaenda kumkamata alipokuwa anaishi wakakagua simu zake , kompyuta na nyaraka nyingine wakapata picha zote kama ushahidi na sasa hivi huyu kijana yuko jela .


Huko mitaani kuna kina betty wengi wamezushiwa , wamedhalilishwa , wamepakaziwa na kutengenezewa habari nyingi mbaya na za kuumizwa na watu wanaowajua au kutowajua lakini wanakaa kimya lakini madhara yake ni makubwa tu .


Inawezekana una ndugu yako , jamaa yako , wewe mwenyewe au mtu mwingine yoyote umeona amedhalilishwa au anataka kudhalilishwa , ni vizuri utoe taarifa kwenye vyombo husika ili wafanyie kazi kwa haraka na mapema zaidi kabla ya tukio kuwa kubwa zaidi .

Unachotakiwa kujua ni kwamba mawasiliano yote kuanzia simu , facebook , watsup , instagram na mengine mengi yanahifadhiwa , hata kama mtu alifuta , kampuni inayotoa huduma husika huwa inasehemu yake ya kuhifadhi mawasiliano yote .


Tushirikiane pamoja ili kuweza kumaliza au kupunguza tatizo hili la unyanyasaji kwa kutumia vyombo vya mawasiliano ili tuweze kuwa na jamii iliyostarabika kwenye mitandao haswa ya kijamii na watu waweze kutumia mitandao hii kwa faida na uhuru zaidi bila kuogopa au kuogopana .


YONA FARES MARO

0786 806028

 



--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.